Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WAITALIANO WATANO WAFARIKI WAKATI WA KUPIGA MBIZI KWENYE MAPANGO YA KISIWA CHA MALDIVES

WAITALIANO WATANO WAFARIKI WAKATI WA KUPIGA MBIZI KWENYE MAPANGO YA KISIWA CHA MALDIVES

 

Raia watano wa Italia wamefariki katika ajali ya kupiga mbizi (scuba diving) katika kisiwa cha Maldives, wizara ya mambo ya nje mjini Roma imesema.

Wizara hiyo imesema waogeleaji hao wanaaminika kufariki wakati wakijaribu kuchunguza mapango katika kina cha mita 50 (futi 164), tukio lililotokea katika eneo la Vaavu Atoll.

Jeshi la Maldives limesema mwili mmoja umepatikana ndani ya pango lililoko takriban mita 60 chini ya maji, huku waogeleaji wengine wanne wakiaminika bado wako eneo hilo.

Limesema waokoaji wenye vifaa maalum wametumwa eneo la tukio, likieleza kuwa operesheni ya utafutaji ni ya hatari kubwa sana.

Tukio hilo linaaminika kuwa ajali mbaya zaidi ya kupiga mbizi kuwahi kutokea katika taifa hilo dogo la Bahari ya Hindi, ambalo ni kivutio kikubwa cha watalii kutokana na visiwa vyake vya matumbawe.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya eneo hilo, Waitaliano hao waliingia majini Alhamisi asubuhi.

Wafanyakazi wa boti ya kupiga mbizi waliokuwa wakisafiri nao waliripoti kutoweka kwao baada ya kushindwa kurejea juu ya maji kwa wakati uliotarajiwa.

Polisi walisema hali ya hewa ilikuwa mbaya katika eneo hilo, takriban kilomita 100 kusini mwa mji mkuu Malé, na onyo la njano lilitolewa kwa boti za abiria na wavuvi

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3