WANANCHI KAGERA WATAKIWA KULINDA MIUNDOMBINU YA BARABARANI
Na Anold Deogratias Matukio Daima Media Kagera
Wananchi mkoani Kagera wametakiwa kutunza na kulinda miundombinu ya barabarani ikiwemo vibanda vya kupumzikia abiria ili vidumu kwa muda mrefu.
Wito huo umetolewa na Meneja wa wakala wa barabara nchini TANROADS mkoa wa Kagera Mhandisi Samwel Mwambugu wakati akizungumza na wanahabari ambapo ameeleza kuwa serikali inatumia gharama kubwa kujenga na kuboresha miundombinu hiyo, hivyo inahitajika kutunzwa na kuangaliwa kwa umakini.
"serikali inatumia gharama kubwa kujenga miundombinu hii kama sheld za kupumzikia, labda kikubwa ambacho ningewaomba wananchi ni kuendelea kuzilinda sheld hizi kama sehemu ya barabara ili zidumu kwa muda mrefu".
Katika hatua nyingine Mhandisi Mwambugu ameeleza kuwa wataendelea kujenga vibanda vya kupumzikia abiri katika maeneo ya miji na katika sehemu ya barabara yenye watu wengi ili kuwapunguzia adha abiria kupigwa na jua au kunyeshewa na mbua, wakati wakisubiri usafiri.
"tutaendele kujenga sheld hizi katika maeneo ya miji na senta kubwa, na tiyari kwa sasa tumejenga katika eneo la Rwamishenye, Nkindo na Kemondo ili kuendelea kuwapunguzia adha abiria"
Kwa upande wao baadhi ya wananchi mkoani Kagera Projestus Ponsian amemshukuru kwa kujengwa kwa vibanda hivyo kwani vinawapunguzia adha ya jua na mvua.
"tunashukuru kujengwa kwa vituo hivi vinatisaidia kujikinga na jua na mvua ni vizuri inasaidia abiria kupata sehemu ya kupumzikia wakati wanasubiri usafiri maana wengine wanatoka huko wamechoka".
Naye Simon Butamanya ameshauri kila eneo ambapo abiria wanasubiri usafiri viwekwe vipanda vya kupumzikia ila kuwakinga abiria na jua wakati wanasubiri magari.
"kwa kweli serikali imejitahidi sana kwa kujengea vituo hivi itatusaidia sisi abiria wakati tunsafiri tunapata sehemu ya kupumzikia na kwa namna hii ningependa kila kituo kijengewe kibanda kama hiki wajikinge na mvua na jua".
Hii ni kwa mara ya kwanza mkoani Kagera kujengwa vibanda vya kupumzikia abiria katika barabara kuu ya Bukoba-Biharamulo.




