Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
HALI YA MAZAO YAWAFURAHISHA WAKULIMA MKOANI IRINGA

HALI YA MAZAO YAWAFURAHISHA WAKULIMA MKOANI IRINGA


Na Easter Kameta (UoI), Matukio Daima Media 

Wakulima mkoani Iringa wa  wameeleza kufurahishwa na hali ya mvua zinazoendelea kunyesha kwa wastani, hali iliyochochea ustawi mzuri wa mazao mashambani na kuleta matumaini ya mavuno bora msimu huu.

Akizungumza na Matukio Daima Media, mkulima Pascal Shaban alisema furaha yake inatokana na maendeleo mazuri ya mazao, tofauti na ilivyokuwa mwaka jana. Alitaja mazao ya mahindi na maharage kuwa yameonyesha ustawi mkubwa kutokana na mvua za kutosha zinazoendelea kunyesha mara kwa mara bila madhara.

“Mahindi na maharage mwaka huu ni mazuri sana na yanaridhisha hali hii inatokana na uwepo wa mvua za kutosha zisizo na vurugu,” alisema Shaban.

Kwa upande wake, Telesia Chalamila alisema kiwango cha mvua kilichopo sasa ni cha wastani na kinaashiria msimu mzuri wa mavuno kwa wakulima wengi mkoani humo. 

Alieleza kuwa mvua hizo zimewezesha mazao kukua kwa ubora wa hali ya juu na kuvutia, jambo linalotarajiwa kuongeza uzalishaji.

“Mwaka huu mvua ziko wastani na zinasaidia mazao kustawi vizuri. Tuna matumaini ya kuvuna mazao mengi ukifika wakati wa mavuno,” alisema Chalamila.

Naye Faidhana Chelesi alilinganisha hali ya mwaka huu na mwaka jana, akisema kuwa msimu huu ni nafuu zaidi kwa wakulima. Alieleza kuwa mwaka uliopita kulikuwapo na upungufu wa mvua uliosababisha baadhi ya mazao kusinya na mengine kukauka kabisa.

“Mwaka jana mvua hazikuwa za kutosha, mazao mengi yaliharibika. Lakini mwaka huu hali ni nzuri zaidi kwa mkulima,” alisisitiza.

Aidha, Fadhili Mwambene alisema mwaka uliopita baadhi ya mazao hayakuota kabisa, huku mengine yakishindwa kukua kutokana na jua kali na ukosefu wa mvua za kutosha. Hali hiyo ilisababisha upungufu wa chakula wakati wa mavuno.

kuwa hali hii ya mvua kwa wakulima mkoani Iringa imekuwa nzuri na  wana matumaini makubwa ya kupata mavuno mengi mwaka huu kutokana na hali nzuri ya mvua inayoendelea kushuhudiwa, tofauti na changamoto za msimu uliopita.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3