Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
KIUWASA KUFUNGA MITA JANJA KWA WATEJA WAKE

KIUWASA KUFUNGA MITA JANJA KWA WATEJA WAKE

 


Mfano wa mita janja za maji (Pre Paid) ambazo zinatarajia kufungwa kwa wateja wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Kigoma (KIUWASA)

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MAMLAKA ya maji safi na usafi wa mazingira Kigoma Ujiji (KIUWASA) imeanza  mpango wa kufunga  mita za maji za malipo ya awali (Pre Paid) ikiwa ni utekelezaji wa mpango mkakati wa mamlaka hiyo katika kuongeza mapato na kuboresha utoaji huduma kwa wateja wake.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KIUWASA,Philipo Funga alisema hayo akitoa taarifa ya mpango wa bajeti wa mamlaka hiyo ya mapato na matumizi kwa mwaka 2026/2027 kwa wajumbe wa kamati ya ushauri ya wilaya Kigoma na kwamba kwa kuanzi mita 100 zitafungwa kwa taasisi mbalimbali za serikali kuanzia mwishoni mwa mwezi huu.


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KIUWASA,Philipo Funga akiwasilisha kwa wajumbe wa kamati ya ushauri ya wilaya Kigoma mpango wa bajeti wa mapato na matumizi ya mamlaka hiyo kwa mwaka 2026/2027

Funga alisema kuwa baada ya utekelezaji huo kuanza mwishoni mwa mwezi huu wanatarajia pia kununua na  kufunga mita za malipo ya awali 1000 kupitia bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027 mpango ambao utatekelezwa kupitia fedha kutoka wizara ya maji lakini pia wameshafanya mazungumzo na wadau mbalimbaali ambao wameonyesha nia ya kuunga mkono mpango huo.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KIUWASA,Philipo Funga akiwasilisha kwa wajumbe wa kamati ya ushauri ya wilaya Kigoma mpango wa bajeti wa mapato na matumizi ya mamlaka hiyo kwa mwaka 2026/2027


Akitoa makisio ya bajeti ya mapato na matumizi kwa mwaka 2026/2027 Mkurugenzi huyo alisema kuwa mamlaka hiyo inatarajia kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 16.3 ambapo kati ya hizo shilingi bilioni 9.5 zitatumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya kuboresha miundo mbinu na utoaji huduma.

Akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa wilaya Kigoma, Dk.Rashid Chuachua alisema kuwa manispaa ya Kigoma Ujiji kama sura ya mkoa inakua kwa kasi kwa shughuli mbalimbali za uchumi na biashara ikiwemo viwanda hivyo uboreshaji wa upatikanaji wa maji ya uhakika ni jambo muhimu na kuomba wabunge kusaidia kusukuma maombo hayo ili fedha za kutekeleza mipango hiyo zipatikane.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3