Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
POLISI KAGERA YAWASHIKILIA WATU 27 KWA TUHUMA ZA VITENDO VYA UHALIFU NA WIZI

POLISI KAGERA YAWASHIKILIA WATU 27 KWA TUHUMA ZA VITENDO VYA UHALIFU NA WIZI

 

Na Anold Deogratias Matukio Daima Media Kagera

Jeshi la polisi mkoani Kagera linawashikilia watuhumiwa 27 kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uhalifu na wizi wa pikipiki, mitumbwi na magari yaliyoibiwa katika nchi jirani na kuingizwa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Kagera Blasius Chatanda ameleeza kuwa watu hao wamekamatwa katika oparasheni maalumu iliyoendeshwa na jeshil la polisi kwa mwezi wa tatu na mwezi wa nne.

Chatanda ameeleza kuwa katika oparesheni hiyo wamefanikiwa kukamata pikipiki 20 za wizi ambapo watuhumiwa 18 wanashikiliwa kwa wizi huo, pia wamekamata magari matatu yaliyoibiwa katika nchi ya Uganda ambapo watuhumiwa wawili wanashikiliwa.

“pia tumekamata magari matatu ya wizi yaliyoibiwa nchi jirani ya Uganda na tunawashikilia watu wawili kwa kujihusisha na wizi huo”


Aidha Kamanda huyo ameeleza kuwa wanawashikilia watuhumia wa 7 kwa wizi wa mitumbwi mitatu kati ya mitano iliyoibiwa iliyokuwa inashikiliwa na jeshi la polisi kwa kujihusisha na uvuvi haramu katika ziwa Victoria ambapo miongoni mwao wapo maafisa uvuvi.

“katika wizi huo wa mitumbwi tunawashikilia walinzi wawili, maafisa uvuvi watatu na watu wengine 2 kwa wizi wa mitumbwi hiyo iliyokuwa imekamatwa na jeshi la polisi kwa kujihusisha na uvuvi haramu, na watuhumiwa wa mitumbwi miwili mingne bado tunawatafuta”


Katika hatua nyingine Kamanda huyo ameeleza kuwa katika mashauri yaliyopelekwa mahakamani watu kumi na wawili  wametiwa  hatiani na kuhukumiwa miaka 30 jela, na watu watano wamehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kubaka, pia watu wawili wamehukumiwa miaka 30 jela na mtuhumiwa mmoja akihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kulawiti.

“kwa mashauri yaliyopelekwa mahakamani watu kumi na wawili  wametiwa  hatiani na kuhukumiwa miaka 30 jela, na watu watano wamehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kubaka, pia watu wawili wamehukumiwa miaka 30 jela na mtuhumiwa mmoja akihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kulawiti”


Kwa makosa ya mauaji watu watano wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la mauaji  huku watu wawili wakihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kukutwa na madawa ya kulevya.

Hata hivyo Kamanda huyo wa jeshi la polisi mkoa wa Kagera amewasihi wanaume mkoani Kagera kuacha kujichukuliwa sheria mkononi hasa mauaji kwa sababu za wivu wa mapenzi ambao umekuwa ndio chanzo kikubwa cha mauaji mkoani  Kagera.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3