TAIWAN INAFUATILIA MABADILIKO YA UONGOZI WA KIJESHI WA CHINA 'YASIYO YA KAWAIDA'
Jan 26, 2026
Taiwan inafuatilia kile ilichokiita mabadiliko "yasiyo ya kawaida" katika uongozi wa kijeshi wa China baada ya jenerali wake mkuu kuanza kuchunguzwa, na kusema kuwa itaendeleza ulinzi wake kwani kiwango cha tishio bado kiko juu, waziri wa ulinzi amesema.China ilitangaza Jumamosi kwamba Zhang Youxia, naibu mkuu chini ya Rais Xi Jinping ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa Tume Kuu ya Jeshi, na afisa mwingine mwandamizi, Liu Zhenli, kuwa wanachunguzwa kwa tuhuma za ukiukaji mkubwa wa nidhamu na sheria."Tutaendelea kufuatilia kwa karibu mabadiliko yasiyo ya kawaida katika ngazi ya juu ya chama cha China, serikali, na uongozi wa kijeshi wa China.Msimamo wa jeshi unatokana na kuwa China haijawahi kuondoa uwezekano wa kutumia nguvu dhidi ya Taiwan," Waziri wa Ulinzi wa Taiwan Wellington Koo aliwaambia waandishi wa habari bungeni.Zhang ameonekana kwa muda mrefu kama mshirika wa karibu wa kijeshi wa Xi, na ni mmoja wa maafisa wakuu wachache wa China wenye uzoefu wa mapigano, baada ya kushiriki katika mzozo wa mpaka na Vietnam wa 1979.China, ambayo inaiona Taiwan inayojitawala kidemokrasia kama eneo lake na hutuma ndege na meli za kivita angani na majini kuzunguka kisiwa hicho karibu kila siku, katika kile ambacho Taipei inakiona kama kampeni ya unyanyasaji ili kuishawishi serikali kukubali madai ya China.