Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
 SHULE YA GOOD VICTORY ENGLISH MEDIUM IRINGA INAVYOVUTIA WAZAZI KWA UBORA WAKE WA ELIMU NA MALEZI.

SHULE YA GOOD VICTORY ENGLISH MEDIUM IRINGA INAVYOVUTIA WAZAZI KWA UBORA WAKE WA ELIMU NA MALEZI.


NA MATUKIO DAIMA MEDIA 

MKOA wa Iringa umeendelea kufanya vema Katika elimu kwa kuwa na vyuo vikuu,vyuo vya kati vingi lakini kuwa na shule za sekondari na shule za Msingi nyingi tena binafsi ambazo zinafanya vizuri Sana na miongoni mwa shule hizo ni pamoja na Good Victory English Medium iliyopo Kata ya Isakalilo Manispaa ya Iringa.

Shule hii imekuwa kimbilio la wazazi na walezi wengi ndani na nje ya mkoa kupeleka watoto wao kupata elimu Bora. 

Good Victory English Medium School ni shule ambayo imejijengea jina kubwa kutokana na matokeo bora ya kitaaluma, malezi imara na uwekezaji mkubwa katika mazingira salama na ya kisasa kwa ukuaji wa mtoto.

 Kwa miaka kadhaa sasa, shule hii imekuwa kivutio kikubwa kwa wazazi kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Iringa wanaotafuta elimu yenye ubora wa juu na matokeo halisi.

Shule ya Good Victory English Medium ilisajiliwa rasmi mwaka 2018 chini ya namba EM 17702, ikianza safari yake kwa lengo la kutoa elimu bora ya awali na msingi kwa kutumia lugha ya Kiingereza.

 Tangu kuanzishwa kwake, shule imejiwekea misingi thabiti ya kumlea mtoto kwa kuzingatia vipengele vitatu vikuu elimu ya kitaaluma, malezi ya kimaadili na maandalizi ya stadi za maisha. 


Msingi huu umeifanya shule kukua kwa kasi na kuaminiwa na wazazi wengi zaidi kila mwaka.

Moja ya sababu kubwa zinazoifanya Good Victory English Medium School kung’ara ni rekodi yake ya kipekee ya ufaulu katika mitihani ya taifa. 

 Mwaka 2024 shule iliandika historia baada ya wanafunzi wake wa Darasa la Saba kushika nafasi ya kwanza Tanzania Bara na Visiwani, kwa kupata asilimia 99.99 ya ufaulu katika Mtihani wa Taifa. 

Mafanikio haya yaliifanya shule kutambulika kitaifa kama mfano wa ubora katika elimu ya msingi.

Toka  mwaka 2019, shule  hii imekuwa ikifanya vizuri mfululizo katika mitihani ya Darasa la Nne na la Saba, hali iliyoiweka katika orodha ya shule bora mkoani Iringa na hata nchini kwa ujumla. 

Matokeo haya si ya bahati mbaya, bali ni matokeo ya mipango madhubuti ya ufundishaji, ufuatiliaji wa karibu wa maendeleo ya mwanafunzi na ushirikiano mzuri kati ya walimu, wanafunzi na wazazi.


Akizungumza kuhusu mafanikio ya kitaaluma ya shule, Mwalimu wa Taaluma, Amos Koneri Kimolimoli, anabainisha kuwa shule inatumia mbinu mseto za ufundishaji zinazolenga kumfikia kila mwanafunzi kulingana na uwezo wake. 

Mbinu hizo ni pamoja na matumizi ya teaching aids, picha, vielelezo, mafunzo shirikishi na mbinu bunifu zinazochochea fikra za wanafunzi.

“Tunatambua kuwa watoto hawajifunzi kwa namna ileile ndiyo maana tunatumia njia tofauti ili kila mwanafunzi apate fursa ya kuelewa na kufanya vizuri,” anasema Mwalimu Kimolimoli.

 Mbinu hizi zimechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza uelewa wa wanafunzi na kuboresha matokeo yao darasani na katika mitihani ya kitaifa.

Mbali na masomo, Good Victory English Medium School imejikita sana katika malezi na nidhamu ya watoto. 

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Sabatho Joashua, anasema kuwa siri ya mafanikio ya shule ni kumjua mtoto mmoja mmoja — tabia zake, uwezo wake na changamoto zake. 

Kupitia mfumo huu, shule huweza kumsaidia mtoto kikamilifu, si kitaaluma tu bali pia kimaadili na kisaikolojia.


Uongozi wa shule unaamini kuwa mtoto mwenye hofu ya Mungu hujenga nidhamu njema, na nidhamu hiyo humsaidia kufanya vizuri shuleni na katika maisha kwa ujumla.

 Kutokana na imani hiyo, shule huendesha vipindi vya dini mara moja kwa wiki, na wanafunzi hupelekwa kanisani au msikitini kulingana na imani zao. 

Kwa wanafunzi wa bweni, usafiri maalum wa shule hutolewa siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kwa ajili ya ibada.

Katika dunia ya leo inayoongozwa na teknolojia, Good Victory English Medium School imewekeza kwa kiwango kikubwa katika ufundishaji wa TEHAMA (Teknolojia ya Habari na Mawasiliano).

 Kila darasa hupata angalau vipindi viwili vya kompyuta kwa wiki, jambo linalomfanya mwanafunzi mmoja kupata zaidi ya vipindi 40 vya kompyuta kwa mwaka. Lengo ni kuhakikisha wanafunzi wanahitimu wakiwa na ujuzi wa msingi wa matumizi ya teknolojia.

Aidha, shule hutoa mafunzo ya kilimo na bustani kupitia shamba darasa, mafunzo ya mapishi kila Jumamosi, elimu ya kazi za mikono na stadi mbalimbali za maisha.

 Programu hizi zimekusudiwa kumwandaa mtoto awe mwenye kujitegemea, mbunifu na anayeweza kukabiliana na changamoto za maisha ya kila siku.

Good Victory English Medium School ina mazingira salama na rafiki kwa mtoto, yakiwa na miundombinu ya kisasa. 

Shule imefungwa mfumo wa kamera (CCTV) katika madarasa, mabweni na maeneo ya wazi ili kuhakikisha usalama wa watoto muda wote. Mabweni ya shule yana utaratibu mzuri wa malezi na hutoa milo mitano kwa siku, ikiwemo matunda kila siku jioni.

Shule pia ina madarasa ya kisasa, uwanja mpana wa michezo na huduma za afya ndani ya shule. 

Mkurugenzi wa shule hiyo, Eunice Kimath, anasema shule imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu. 

Kupitia mpango maalum wa kijamii, zaidi ya watoto 50 wamenufaika kwa kulelewa na kusomesha bure au kwa gharama nafuu, ikiwa ni sehemu ya mchango wa shule katika maendeleo ya jamii.

Kimath anatoa wito kwa wazazi wote wanaotafuta shule yenye elimu bora, uangalizi wa karibu na malezi ya kina, kuichagua Good Victory English Medium School. 

“Tunapokea watoto wa dini zote na kutoka maeneo yote ya Tanzania tunamlea mtoto kiakili, kimwili, kimaadili na kiufundiha hapa ni mahali salama pa ukuaji wa mtoto wa Kiafrika,” anasema.

Ni ukweli kuwa kwa misingi ya nidhamu, elimu bora, matumizi ya teknolojia, malezi thabiti na mazingira salama, Good Victory English Medium School imeendelea kuwa kielelezo cha ubora wa elimu nchini. 

Jackson Sanga ni mkazi wa Iringa mjini ambae watoto wake wawili wanasoma Katika shule hiyo anasema sababu ya kusomesha hapo ni kutokana na kiwango kizuri cha ugundishaji pia pamoja na kuwa ada ni Msingi wa elimu Bora Ila shule haisumbui wazazi kama ilivyomaeneo mengine. 


Huku Wema Kyando mbali ya kupongeza ubora wa shule hiyo bado aliomba upngozi wa shule hiyo kuwa na ndoto ya kuanzisha sekondari ama chuo ili mtoto akianza elimu ya Msingi ajiunge na sekondari Hadi chuo. 

Historia yake ya matokeo bora imekuwa ikiwavuta wazazi wengi kuhamisha watoto wao kutoka shule nyingine ndani na nje ya Mkoa wa Iringa na kuwapeleka Good Victory, shule inayothibitisha kuwa uwekezaji katika elimu bora huzaa matokeo chanya ya kudumu.

 


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3