Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
 CCM YAWEKA WAZI SABABU ZA KUTOTUMIA UWANJA  WA SAMORA KATIKA MAZISHI YA EDO BASHIRI

CCM YAWEKA WAZI SABABU ZA KUTOTUMIA UWANJA WA SAMORA KATIKA MAZISHI YA EDO BASHIRI


NA MATUKIO DAIMA MEDIA.

Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa kimeeleza kuwa matumizi ya Uwanja wa Samora kwa ajili ya shughuli za kumuaga aliyekuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Iringa, marehemu Eddo Bashiri, yalitokana na makubaliano kati ya viongozi wa chama na familia ya marehemu.

Akizungumza wakati wa shughuli za kumuaga marehemu, Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa Daudi Yasin alisema mara baada ya kupata taarifa za msiba, sekretarieti za CCM Mkoa na Wilaya zilifanya mazungumzo na familia kwa lengo la kupanga namna ya kumpumzisha marehemu.

Alisema familia ndiyo iliyopendekeza shughuli za kumuaga marehemu zifanyike katika uwanja wa KKKT Kibwabwa  kutokana na uwepo wa ndugu na wananchi wengi waliokuwa wamekusanyika Iringa, pamoja na mazingira ya msiba uliokuwa nyumbani kwa marehemu eneo la kibwabwa.

Aidha, alifafanua kuwa Uwanja wa Samora ni mali ya CCM na kwamba familia ndiyo iliyowaelekeza viongozi wa chama kutumia uwanja wa KKKT  kwa ajili ya shughuli hiyo, akisisitiza kuwa chama kilikuwa na wajibu wa kumuenzi kiongozi wake kutokana na mchango wake.

Alisema CCM inatambua na kuheshimu kazi kubwa alizozifanya Edo Bashiri ndani ya chama na katika shughuli mbalimbali za kijamii, hivyo haikuwa na sababu ya kukataa ombi la kutumia uwanja huo kwa ajili ya kumuaga Eddo.

MWISHO.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3