MAGAZETINI LEO JUMATANO NOVEMBA 25.2026:MTANGAZAJI NGULI EDO BASHIRI AFARIKI DUNIA,WANANCHI WAOMBA MWILI WAKE UAGWE UWANJA WA SAMORA
Nov 24, 2026
mwanahabari Edwin Bashiri Sanga amefariki dunia katika Hospitali ya misheni Ikonda alikokuwa akitibiwa . Edwin alikuwa mtangazaji wa Radio Ebony Fm na ndio radio iliyomheshimisha zaidi na kumtambulisha kwa jamii na kuwa na umaarufu mkubwa . pia mbali ya kuwa mtangazaji hadi kifo chake alikuwa mwemezi wa CCM wilaya ya Iringa mjini .
Baadhi ya wananchi waliozungumza na Matukio Daima kufuatia kifo hicho wamesema kutokana na umaarufu wa Edo wanaomba mwili wake uagwe uwanja wa Samora ili kutoa nafasi ya wananchi wengi kumuaga mpendwa wao.
Msiba wa Edo umetengwa eneo la Kitwiru kwa mlezi wake marehemu Sanga aliyefariki mapema mwaka huu .









































