Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MCC SALIM ASAS AAHIDI KUSAIDIA FAMILIA YA EDDO BASHIR

MCC SALIM ASAS AAHIDI KUSAIDIA FAMILIA YA EDDO BASHIR

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA

IRINGA.Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Salim Abri Asas ameahidi kutoa mchango wa kusaidia familia ya aliyekuwa Mtangazaji maarufu wa Redio mkoani Iringa, Edwin Bashiri Sanga maarufu kama Eddo, aliyezikwa jana  Novemba 26, 2026.

Akitoa ahadi hiyo, Asas amewataka Wananchi kujenga utamaduni wa kusaidiana na kuthaminiana wakati wa uhai wao, badala ya kusubiri hadi Mtu anapofariki dunia ndipo waonyeshe upendo na mshikamano.

Aidha, Asas amesisitiza umuhimu wa Jamii kushirikiana katika nyakati za furaha na changamoto, akieleza kuwa msaada unaotolewa wakati Mtu akiwa hai una umuhimu mkubwa katika kuboresha maisha yake na ya Familia yake.

Alisema aliwahi kumtembelea marehemu alipokuwa amelazwa katika Hospitali ya Frelimo akiwa ameambatana na Katibu wa Wilaya na viongozi wengine, akisisitiza kuwa utamaduni huo unapaswa kuendelezwa kwa vitendo.

Aidha, alieleza kuwa marehemu alikuwa na mchango mkubwa ndani ya CCM na katika shughuli za kijamii, hivyo chama kina wajibu wa kuendelea kuienzi familia yake hata baada ya mazishi.

Aliongeza kuwa marehemu alikuwa mwanahabari na mtu mwenye moyo wa kujitolea, aliyekuwa akitumia nafasi yake kusaidia watu wenye mahitaji mbalimbali, wakiwemo wagonjwa hospitalini na mahabusu.

MWISHO

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3