Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
KIGOMA YATANGAZA MAFANIKIO UDHIBITI WA EBOLA

KIGOMA YATANGAZA MAFANIKIO UDHIBITI WA EBOLA


 MKOA Kigoma unaelezwa kupiga hatua kubwa katika kudhibiti kuingia kwa ugonjwa wa Ebola ambao kwa sasa umesababisha idadi kubwa ya vifo katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na kwamba kwa sasa hakuna mgonjwa aliyeripotiwa mkoani humo.


MKUU wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro akizungumza katika kikao cha wadau wa afya kutathmini hatua zilizochukuliwa kudhibiti ugonjwa huo alisema kuwa pamoja na mafanikio hayo hatua Zaidi za kudhibiti hali hiyo zimeendelea kutekelezwa.


Katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya Kigoma, Dk.Rashid Chuachua alisema kuwa malengo na mikakati iliyowekwa imefanya kazi na kuufanya mkoa huo kuwa salama hadi sasa ambapo ametoa wito kwa wataalam wa afya na wadau mbalimbali kuhakikisha hatua Zaidi zinachukuliwa kuhakikisha ugonjwa huo hauingii mkoani humo sambamba na kuwataka kila moja kutoa taarifa anapoona kuna mtu mwenye dalili ya mgonjwa.


 Akitoa taarifa kwa wajumbe wa kikao hicho hatua mbalimbali zilizochukuliwa na timu ya afya ya mkoa, Mratibu wa magonjwa ya mlipuko mkoa Kigoma, Albert Paschal alisema kuwa hatua muhimu za kudhibiti ugonjwa huo zimetekelezwa na kufanikisha kuufanya mkoa huo kubaki salama hadi sasa ikiwemo kutoa elimu kwa wahudumu wa afya mkoani humo.


Paschal alizitaja hatua nyingine zilizochukuliwa ni pamoja na kufanya ufuatiliaji katika mipaka yote inayoingia mkoani humo, mkoa umeanzisha maabara tembezi ya vipimo, mipaka isiyo rasmi imetambuliwa na viongozi wa vijiji wamepewa elimu na maelekezo ya kutoa taarifa za dalili ya mgonjwa na kwenye baadhi ya mipaka yenye idadi kubwa ya wasafiri kumefungwa vifaa vya kupima joto la wagonjwa sambamba na uwepo wa utayari wa magari ya kubeba wagonjwa (Ambulance).


Pamoja na hatua hiyo Katibu wa CCM mkoa Kigoma,Christopher Pallangyo amepongeza hatua za udhibiti wa ugonjwa huo mkoani Kigoma akitaka pia hatua Zaidi zichuliwe kwenye vizuizi mbalimbali vya barabarani kwa kuwepo kwa watoa huduma za afya ambap pia wataratibu zoezi la kukagua watu wanaopita maeneo hayo.




Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3