Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
SEKTA YA UCHUKUZI NI MHIMILI WA UCHUMI, NIT YAONGEZA UWEZO WA KUZALISHA WATAALAMU

SEKTA YA UCHUKUZI NI MHIMILI WA UCHUMI, NIT YAONGEZA UWEZO WA KUZALISHA WATAALAMU

 

Na Hamida Ramadhan,Matukio Daima Media, Dodoma

SEKTA ya uchukuzi imeelezwa kuwa mhimili muhimu wa maendeleo ya uchumi wa taifa, huku Serikali ikiendelea kuimarisha Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ili kuzalisha wataalamu wenye ujuzi wa kuendesha na kusimamia miundombinu ya kisasa ya usafirishaji nchini.


Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi Dkt. Prosper Mgaya, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Mtumba, jijini Dodoma.

Dkt. Mgaya alisema NIT imeendelea kupanua programu za mafunzo ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya wataalamu katika sekta za usafiri wa barabara, reli, anga na majini, kufuatia uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika miundombinu ya uchukuzi.


Ameeleza kuwa chuo hicho kilianzishwa mwaka 1975 kama kitengo cha Shirika la Usafirishaji la Taifa, kabla ya kupandishwa hadhi mwaka 1982 kuwa taasisi ya elimu ya juu yenye jukumu la kutoa mafunzo, kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu katika sekta ya uchukuzi.


Amesema baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977, Tanzania ilikabiliwa na upungufu wa wataalamu wa sekta ya uchukuzi, hali iliyoifanya Serikali kuimarisha NIT ili kuzalisha wataalamu watakaokidhi mahitaji ya taifa.

Aidha, amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanyika katika Reli ya Kisasa (SGR), ununuzi wa ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), ujenzi na ukarabati wa meli pamoja na uboreshaji wa viwanja vya ndege, akisema miradi hiyo imeongeza mahitaji ya wataalamu wenye ujuzi wa hali ya juu.


Amesisitiza kuwa NIT itaendelea kuboresha mitaala na mafunzo ya vitendo ili kuandaa wahitimu wenye uwezo wa kukidhi mahitaji ya soko la ajira na kuchangia maendeleo endelevu ya sekta ya uchukuzi na uchumi wa taifa.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3