Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
 MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA NJOMBE, BALOZI DKT. PINDI CHANA ASHIRIKI MAFUNZO YA WAKULIMA KUHUSU VIPIMO

MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA NJOMBE, BALOZI DKT. PINDI CHANA ASHIRIKI MAFUNZO YA WAKULIMA KUHUSU VIPIMO

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA ,NJOMBE 

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe, Balozi Dkt. Pindi Chana amepongeza mafunzo ya kuwajengea uwezo  wakulima mkoa wa Njombe .


 Kuwa mafunzo hayo yaliyolenga kuwajengea uwezo kuhusu matumizi sahihi ya vipimo katika shughuli za kilimo na biashara ya mazao ni nyenzo muhimu kwa wakulima hao.

kuwa katika mafunzo hayo yamefanyika mkoani Njombe kwa ushirikiano wa wataalamu wa sekta ya vipimo pamoja na wadau mbalimbali wanaohusika na maendeleo ya kilimo yanapaswa kutolewa mara kwa mara 

Akizungumza baada ya kushiriki mafunzo hayo, Balozi Dkt. Pindi Chana alisema elimu ya matumizi sahihi ya vipimo ni muhimu kwa wakulima kwa kuwa inawasaidia kufanya biashara kwa uaminifu, kuongeza tija na kuhakikisha wanapata thamani halisi ya mazao yao. 

Alieleza kuwa matumizi ya vipimo vilivyothibitishwa huchangia kuondoa migogoro kati ya wauzaji na wan


unuzi, huku yakiongeza uwazi katika biashara.

"Nimetoka kushiriki mafunzo hapa Njombe yaliyowaleta pamoja wakulima na wataalamu wa vipimo. Mafunzo haya yamekuwa na manufaa makubwa kwa sababu yamewapa wakulima uelewa wa haki zao na wajibu wao katika matumizi ya vipimo vinavyokidhi viwango vinavyotambuliwa," alisema.

Aidha, aliwapongeza wataalamu wa vipimo kwa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi, akieleza kuwa hatua hiyo inasaidia kujenga uchumi wa wakulima kupitia biashara yenye kuzingatia sheria, usawa na uadilifu. 

Alisema  kuwa wakulima wanapaswa kuhakikisha wanatumia mizani na vipimo vilivyokaguliwa na kuthibitishwa na mamlaka husika ili kujiepusha na hasara zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya vifaa visivyo sahihi.


Katika mafunzo hayo, washiriki walipata fursa ya kujifunza kuhusu umuhimu wa kukagua mara kwa mara vipimo vinavyotumika katika biashara, namna ya kutambua vipimo vilivyoidhinishwa pamoja na hatua za kuchukua wanapobaini matumizi ya vipimo visivyokidhi viwango. 

Elimu hiyo pia ilihusisha namna matumizi sahihi ya vipimo yanavyochangia kuongeza imani ya wateja na kuboresha ushindani wa bidhaa za wakulima katika soko.

Washiriki wa mafunzo hayo walieleza kufurahishwa na elimu waliyoipata, wakisema itawasaidia kufanya biashara kwa ufanisi zaidi na kulinda maslahi yao.

 Walisema kuwa mara nyingi changamoto za vipimo zimekuwa zikisababisha baadhi ya wakulima kupata hasara, hivyo elimu waliyopewa itawasaidia kufanya maamuzi sahihi na kuhakikisha haki inazingatiwa katika kila hatua ya biashara.

Balozi Dkt. Pindi Chana alisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuweka mazingira bora yanayowawezesha wakulima kuongeza uzalishaji na kupata masoko yenye ushindani kwa kuzingatia viwango na sheria zinazolinda maslahi ya wazalishaji na watumiaji. 

Alisema elimu kama hiyo inapaswa kuwafikia wakulima wengi zaidi ili kuongeza uelewa na kuchochea maendeleo ya sekta ya kilimo.


Kwa upande wao, waandaaji wa mafunzo hayo wameeleza kuwa wataendelea kushirikiana na viongozi wa serikali, taasisi za umma na wadau wa maendeleo kuhakikisha elimu kuhusu vipimo inawafikia wananchi wengi zaidi, hasa wakulima na wafanyabiashara wa mazao.

 Walisema matumizi sahihi ya vipimo ni msingi wa biashara yenye haki na maendeleo endelevu ya uchumi wa wananchi.


Mafunzo hayo yamehitimishwa kwa wito kwa wakulima kuendelea kutumia elimu waliyoipata katika shughuli zao za kila siku, huku wakihamasishwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika pale wanapobaini matumizi ya vipimo visivyo sahihi.


 

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3