Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
 RIJK ZWAAN YAJIVUNIA MBEGU BORA, MASOKO YA UHAKIKA

RIJK ZWAAN YAJIVUNIA MBEGU BORA, MASOKO YA UHAKIKA

Na Hamida Ramadhan,Matukio Daima Media Dodoma

KAMPUNI ya RIJK ZWAAN Tanzania imesema imejikita katika kuwawezesha wakulima kwa kuwapatia mbegu bora za mboga, elimu ya kilimo cha kisasa na kuwaunganisha na masoko ya uhakika ili kuongeza tija na kipato.

Akizungumza katika Maonesho ya 33 ya Kimataifa na Kitaifa ya Kilimo (Nanenane) yanayoendelea katika Viwanja vya Maonesho ya wakulima Nzuguni jijini Dodoma, Mtaalamu Mwandamizi wa Maendeleo ya Bidhaa na Afisa wa Kilimo wa kampuni hiyo, Neiman Mollel, amesema lengo la RIJK ZWAAN si kuuza mbegu pekee, bali kuhakikisha mkulima anafanikiwa kuanzia uzalishaji hadi kuuza mazao yake.

Amesema kampuni hiyo inazalisha na kusambaza mbegu bora zinazostahimili mabadiliko ya hali ya hewa, magonjwa na mazingira mbalimbali ya uzalishaji, hatua inayowasaidia wakulima kupata mavuno mengi yenye ubora unaohitajika sokoni.

Mollel amesema kupitia wataalamu wake wa kilimo, kampuni hiyo pia hutoa mafunzo ya matumizi ya teknolojia za kisasa na mbinu bora za uzalishaji ili kuwajengea uwezo wakulima na kuongeza ushindani wa mazao yao katika soko.


Kwa upande wake, mkulima wa Dodoma, Ray Mack, amewahimiza wakulima na vijana wanaotamani kuingia katika kilimo biashara kutembelea shamba la maonesho la RIJK ZWAAN lililopo Nzuguni ili kujifunza kwa vitendo namna ya kuzalisha mazao kwa tija kwa kutumia mbegu bora na teknolojia za kisasa.

Amesema vijana wengi huona ukosefu wa mtaji kuwa kikwazo cha kuanza kilimo, lakini kwa sasa Serikali imeweka mazingira wezeshi kupitia mikopo inayotolewa na halmashauri, taasisi za kifedha na benki, hivyo hakuna sababu ya kuacha kutumia fursa zilizopo.

Ray Mack amesema RIJK ZWAAN mkulima Dodoma inaendelea kushirikiana na wakulima katika mikoa ya Dodoma, Arusha, Morogoro na Mwanza kwa lengo la kukuza kilimo biashara, kuongeza uzalishaji na kuwawezesha wakulima kupata masoko ya uhakika kwa mazao yao

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3