Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
NSSF WAWAFIKIA BODABODA CHUNYA KWA FURSA KUJALI MAISHA YAO.

NSSF WAWAFIKIA BODABODA CHUNYA KWA FURSA KUJALI MAISHA YAO.

 

NA JOSEA SINKALA, MBEYA.

Mfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) ambao hutoa hifadhi ya jamii kwa wanachama walioajiriwa na waliojiajiri sasa imeendelea kutoa elimu na fursa mbalimbali kwa jamii ikiwemo program ya skimu ya Taifa ya hifadhi ya jamii kwa wananchi waliojiajiri ili kuwaendeleza kwenye shughuli za kiuchumi.

Akizungumza mkoani Mbeya afisa mwandamizi wa NSSF kutoka mkoani humo bwana Ibrahim Nganga, amesema katika kufikia maendeleo endelevu na hususani kuelekea dira ya maendeleo ya Taifa mwaka 2050 Serikali kupitia mfuko huo imeamua kulifikia kundi madereva bodaboda katika Halmashauri ya wilaya ya Chunya ili kuwapatia fursa ya kujiunga na mfuko huo kwa ajili ya maisha yao bora ya sasa na baadaye.

Amesema madereva hao hukumbana na changamoto mbalimbali wawapo kazini hivyo kushindwa kumudu utunzaji wa fedha, gharama za matibabu na mahitaji mengine watakayosaidika kutokana na uwekezaji kwenye mfuko huo wa hifadhi ya jamii.


Hata hivyo afisa mwandamizi huyo wa NSSF amewaomba madereva katika maeneo mbalimbali kuchangamkia fursa hiyo kwa faida yao, familia zao na Taifa kwa ujumla ikiwemo kunufaika na pensheni kama za uzeeni, za ulemavu, uzazi na mafao ya matibabu.




Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3