Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
SIRRO ATAKA ZAO LA TUMBAKU LIBORESHE MAISHA YA WAKULIMA

SIRRO ATAKA ZAO LA TUMBAKU LIBORESHE MAISHA YA WAKULIMA


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MKUU wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro ametaka wadau wa zao la tumbaku mkoani Kigoma  kusimamia taratibu za kilimo na uuzaji wa zao hilo ili kuhakikisha mkulima ananufaika na kuwa na maendeleo.


Balozi Sirro alisema hayo akifungua kikao cha wadau wa tumbaku mkoani Kigoma na kusema kuwa wakati zao la tumbaku likielezwa kuwa ni zao la pili kwa kuingiza maapato ya serikali na kuingiza fedha za kigeni bado kauli hiyo haiakisi hali ya wakulima wa tumbaku mkoani Kigoma.

Alisema kuwa kwa sehemu kubwa inaonekana makampuni ya ununuzi wa tumbaku yamekuwa yakineemeka na zao hilo huku wakulima wakilalamika ikiwemo kupunjwa bei lakini pia kuchelewa kwa malipo yao hivyo kurudisha nyuma juhudi za wakulima kujikwamua na kupiga hatua za maendeleo.

 


Kutokana na hilo Mkuu huyo wa mkoa ametaka kila mdau kutumia vizuri nafasi yake ikiwemo watendaji wa serikali, bodi ya tumbaku (TCB), wanunuzi na vyama vya msingi na chama kikuu cha wakulima wa tumbaku (KTCU)

 


Awali akiwasilisha taarifa mbele ya Mkuu wa mkoa katika kikao hicho kaimu Meneja wa kanda ya Magharibi wa Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB), Elisha Chao alisema kuwa Zaidi ya kilo  milioni 15 za tumbaku zinatarajia kununuliwa msimu huu wa mauzo kwa mkoa Kigoma.


Chao alisema kuwa hadi sasa wakati masoko yakiwa yanaendelea tayari kilo milioni 15 zimeshanunuliwa nab ado kuna tumbaku ipo sokono na wanunuzi wakiendelea na taratibu za ununuzi kwenye masoko hayo.

Chao alisema kuwa pamoja na kupanda na kushuka kwa mauzo ya tumbaku nje ya nchi tumbaku imeendelea kuwa moja ya mazao manne inayoingizia serikali fedha za kigeni na kutoa ajira kubwa likiwa na wakulima Zaidi ya 80,000.

Awali Kaimu Katibu Tawala wa mkoa Kigoma, Zao la tumbaku mkoani Kigoma limeendelea kukuwa kutoka tani 4452  mwaka  2021/2022 kufikia tani 14,213 mwaka 2024/2025 hivyo kuongezeka kwa uzalishaji kumeongeza ukusanyaji  wa mapato ya serikali yakitoka Bilioni 15.4 mwaka  2023/2024  na kufikia shilingi bilioni 26.9 kwa mwaka 2025/2026 sawa na ongezeko la asilimia 22 ambapo tumbaku inachangia mapato ya mkoa kwa asilimia 13 likiwa zao la tatu kwa mkoa Kigoma.

Mwisho.



Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3