BODABODA LUPATINGATINGA WAFIKIWA, 'UKIUMIA KICHWA HAKUNA KICHWA BANDIA'.
Na Josea Sinkala, Mbeya.
Huko mkoani Mbeya, madereva wa pikipiki za magurudumu mawili (Bodaboda) wameelezwa kuwa baadhi yao bado ni changamoto katika kutii sheria za usalama barabarani hatua inayochochea kuendelea kutokea kwa ajali zisizo na ulazima na kugharimu maisha ya bodaboda.
Kwa mujibu wa Afande Deo wa kituo cha Polisi Lupatingatinga wilayani Chunya mkoani Mbeya, madereva wengi wamekuwa wakiendesha vyombo vyao kwa uzembe na bila kujijali na kusababisha ajali mbalimbali.
Baadhi ya madereva wanatajwa kutokuwa na leseni, kuendesha pikipiki bila kuvaa kofia ngumu (helmet) huku baadhi wakitumiwa katika matukio ya uhalifu jambo ambalo Polisi imeonya na kuwaomba madereva bodaboda kutokuwa chachu ya uhalifu.
Kwa upande wake kaimu Katibu wa bodaboda wilaya ya Chunya amewashauri madereva wenzako kuacha makusudi na kuzingatia mafunzo ambayo wamekuwa wakipewa mara kadhaa ikiwa ni pamoja na kujitokeza kwenye mafunzo ambayo yamekuwa yakiitishwa kwa faida yao wenyewe.



