Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
 DC MAPUNDA: WAZAZI SIMAMIENI MALEZI YA VIJANA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA

DC MAPUNDA: WAZAZI SIMAMIENI MALEZI YA VIJANA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA

Matukio Daima, Dar 

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixstus Mapunda ameitaka jamii kukataa na  kuongeza usimamizi wa malezi ya vijana ikiwamo kuwapa muda wa kuzungumza nao namna ya kujiepeusha na matumizi ya dawa za kulevya.

Kadhalika amesema jukumu kubwa kwa sasa ni wazazi kuzungumza na vijana wao mapema kukataa kuonja au kujaribu matumizi ya dawa za kulevya ili wasambazaji wakose soko la kuangamiza vijana wa Tanzania.

Alitoa kauli hiyo leo  wakati akifungua Tamasha la kuhamasisha jamii kuhusu madhara ya matumizi ya dawa za kulevya lililofanyika katika viunga vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam.

Alisema katika wilaya yake amepiga marufuku mtindo wa kumwaga fedha nyingi hadharani zinazowapa tamaa vijana wasio na kipato kuhamasika kuingia kwenye mfumo wa kutumia, kusambaza na kuuza dawa za kulevya nchini.

" Wazazi tutenge muda wa kuzungumza na watoto wetu kukataa kujaribu matumizi ya dawa za kulevya mapema ili kujenga vijana Imara... Ndani ya wilaya yangu nimepiga marufuku tabia ya kumwaga fedha hadharani kujenda ushawishi kwa vijana kuingia kwenye mfumo wa dawa za kulevya" alisema Mkuu wa Wilaya Mapunda.

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi Divisheni ya Dawa na Tina, Dk. Cassian Nyandindi akizungumza kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) amesema bado inahitajika elimu sahihi kwa umma kuhusu kukataa kuonja au kujaribu matumizi ya dawa za kulevya nchini.

Amesema jitihada za kutosha zinahitajika kuanzia ngazi ya kaya kwa vijana kuacha matumizi ya dawa za kulevya ili kuimarisha taifa letu.

Mwisho

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3