Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
 BARAZA LA VYAMA VYA SIASA LASISITIZA SIASA ZA MARIDHIANO NA KUWAWEZESHA WANAWAKE

BARAZA LA VYAMA VYA SIASA LASISITIZA SIASA ZA MARIDHIANO NA KUWAWEZESHA WANAWAKE


Na Matukio Daima Media, Morogoro 

Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania limesema litaendelea kuweka mkazo katika kujenga maridhiano miongoni mwa vyama vya siasa pamoja na kuwawezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika uongozi na shughuli za kisiasa nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Juma Ali Khatibu, mara baada ya kuchaguliwa tena kuongoza baraza hilo kwa awamu ya pili katika uchaguzi uliofanyika mjini Morogoro.

Khatibu amesema pamoja na kuendelea kuishauri Serikali kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa, baraza hilo litaendelea kusimamia ajenda ya umoja, mshikamano na amani ili kuhakikisha ushindani wa kisiasa hauwi chanzo cha migogoro.

Aidha amesema baraza hilo litaendelea kuishauri Serikali kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa, ikiwemo namna ya kushughulikia ukiukwaji wa sheria unaofanywa na vyama vya siasa bila kuathiri haki za vyama vingine ambavyo havijahusika.

Kwa upande wake, Saumu Rashid, Katibu Mkuu wa UDP, amesema uchaguzi wa viongozi wa baraza hilo umefanyika kwa uwazi na umeonesha kuwa vyama vya siasa vinaweza kushindana kwa misingi ya kidemokrasia huku vikidumisha mshikamano.

Naye Said Sudi Said, Mwenyekiti wa AAFP, amesema juhudi za Baraza la Vyama vya Siasa katika kuwajengea uwezo wanawake zimeanza kuzaa matunda kwa kuongeza ushiriki wao katika uongozi wa kisiasa, akitaka juhudi hizo ziendelezwe.

Wajumbe wa baraza hilo wameahidi kuendelea kushirikiana katika kulinda amani, umoja na maendeleo ya nchi kupitia majadiliano na ushirikiano kati ya vyama vya siasa.

Mwisho

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3