Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
 VIFO AJALI YA SEKENKE VYAFIKIA WANANE‎

VIFO AJALI YA SEKENKE VYAFIKIA WANANE‎


‎Singida,

‎‎Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ajali ya barabarani iliyohusisha lori na basi dogo aina ya Coaster katika Mlima Sekenke, wilayani Iramba mkoani Singida, imeongezeka kutoka saba hadi kufikia wanane, baada ya mwanaume mmoja majeruhi aliyekuwa akipatiwa matibabu kufariki.

‎‎Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Dk. Peter Luhega, alisema majeruhi 17 waliopatikana katika ajali hiyo waliopokelewa katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba kwa ajili ya matibabu, mmoja amefariki na wengine wameruhusiwa, na kubakia wagonjwa sita pekee hadi sasa.



‎‎Alisema siku ya tikio jumla ya watu saba walikufa, wakiwemo wanaume watano na watoto wawili wa kike, lakini sasa kifo kimoja zaidi cha mwanaume kimeongezeka, hivyo kufanya jumla kuwa wanane waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

‎‎Ajali hiyo ilitokea Juni 2, 2026, majira ya saa 4:00 asubuhi, baada ya lori lililokuwa likishuka Mlima Sekenke kupata hitilafu ya breki na kuligonga kwa nyuma basi dogo la abiria aina ya Coaster lenye namba za usajili DVD 370 lililokuwa likitoka Singida kwenda Igunga mkoani Tabora, kwa kugongana, na magari yote mawili yalitumbukia korongoni kando ya Barabara Kuu ya Singida-Nzega.


‎Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, aliyefika siku hiyo katika eneo la ajali na baadaye hospitali ya wilaya ya Iramba kuwajulia hali majeruhi, alitoa pole kwa serikali ya wilaya Iramba na familia zilizopoteza ndugu zao na kuwatakia nafuu majeruhi. 

‎MWISHO

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3