Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
 USHIRIKA WATAKIWA KULINDA AMANI, KUEPUKA RUSHWA

USHIRIKA WATAKIWA KULINDA AMANI, KUEPUKA RUSHWA


‎‎Singida,

‎‎Wakati vyama vya ushirika vikizidi kuwa mhimili wa maendeleo ya kiuchumi kwa maelfu ya wakulima mkoani Singida, jamii na viongozi wametakiwa kuilinda amani, kuzingatia uadilifu, na kuimarisha maadili mema, ili kuharakisha maendeleo yaliyokusudiwa na Serikali.

‎‎Mwenyekiti wa Ushirika Mkoa wa Singida, Clementi Mkumbo,amesema hayo wakati wa mkutano wa Jukwaa la Maendeleo ya ya Ushirika Mkoa wa Singida mwaka 2026 na kushirikisha vyama vyote vya Ushirika, na wadau wake, wanaounda mnyororo wa thamani ya mazao.


‎‎Mkumbo alieleza kuwa maendeleo ya vyama vya ushirika yanategemea uwepo wa amani na utulivu, akibainisha kuwa migogoro inaweza kudhoofisha juhudi za wakulima na kuathiri mafanikio ya vyama hivyo. Kaulimbiu ya ushirika mwaka 2026 ni, “Ushirika kwa Dunia Yenye Amani, Linda Ushirika Chagua Uadilifu.”


‎Katika jukwaa hilo, Afisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Singida, Benjamin Masagya, aliwataka viongozi wa ushirika kutenganisha maslahi yao binafsi na yale ya wanachama, ili kuimarisha uwajibikaji na kuondoa migogoro ndani ya vyama.

‎‎Alisema viongozi wanaotumia nafasi zao vibaya kwa kujinufaisha wao wenyewe, huweza kuathiri maendeleo ya taasisi wanazoziongoza, na hata kupunguza imani kwa wanachama wa vyama vyao vya ushirika.


‎Mmoja wa washiriki wa jukwaa hilo, Athumani Iddi kutoka Umoja Amcos ya Kata ya Mtoa wilayani Iramba, aliyetaka kufahamu hatua zinazochukuliwa dhidi ya viongozi wanaojilimbikizia mali kwa njia zisizo halali, na kujibiwa kuwa, jukumu la mapambano rushwa ni shirikishi kwa jamii nzima kukataa rushwa pamoja na vishawishi vyote, mahali popote nchini.

‎‎Kaulimbiu ya ushirika mwaka 2026 ni, “Ushirika kwa Dunia Yenye Amani, Linda Ushirika Chagua Uadilifu.”

‎MWISHO

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3