WAUMINI WA KIISILAM WASHAURIWA KUSHIRIKI IBADA YA KUCHINJA NA KUSAIDIA WENYE UHITAJI
NA MATUKIO DAIMA MEDIA.
IRINGA.WAUMINI wa kiisilamu nchini wameshauriwa kushiriki Katika ibada ya kuchinja ibada inayoambatana na siku tukufu ya Eid ya Kuchinja na kutoa sadaka kwa wale wasiojiweza kupata kitoweo katika siku hii ya sikukuu.
Wito
umetolewa katibu Mkuu wa Taasisi ya DHI-Nureyn Islamic Foundation Sheikh Shams
Elmi na kusema kuwa Eid ya kuchinja ilianzishwa na Nabii Ibrahim na mtoto wake
Ismail kwa kutoa muhanga uchinjaji wa wanyama na kutoa sadaka kwa Mwenyezi
Mungu
Shams
alisema kuwa Leo wamechinja Ng’ombe 30 kutoka kwa wafadhili mbalimbali wa ndani
ambao wametekeleza ibada kwa kuchinja mifugo hii ili kurudisha kwa Mwenyezi
Mungu kwa lengo la kuwasaidia waumini ili waweze kufurahia Eid ya kuchinja kwa
furaha kwa kuwapatia kitoweo siku ya leo.
“Sasa hivi tunakagua usalama wa nyama kwa ajili ya kuzifikisha kwa walengwa maeneo tunakayogawa ni vituo vya yatima,nyumba za wajane,maeneo ya walemavu na tutaangalia wale wenye hali ngumu katika maisha na kuwapelekea nyama hizi ikiwa ni sadaka kutoka kwa waislamu”alisema
Aidha Shams alitoa
wito kwa waumini wa dini hiyo kuwa ibada ya kuchinja imesisitizwa katika vitabu
vya dini nan i ibada inayokusudiwa kumuingizia furaha tu ambaye hana uwezo wa
kupata kitoweo siku hii ya Eid.
“Ni wito kwa
jamii yote kwa ujumla kwa kuwa hali ya kiuchumi duniani imeathirika kwa kiwango
kikubwa sana unapojihimiza kutoa sadaka, kuwasaidia watu kwa njia yeyote ni
jambo la heri na kuwapunguzia watu ukali wa maisha”alisema
Alisema kuwa dunia nzima imeathirika kiuchumi awali walikuwa na uwezo wa kuchinja ng’ombe 60 lakini mwaka huu wamechinja ng’ombe 30 kwa sababu ya wafadhili wamerudi nyumba kutokana na hali ya kiuchumi kupanda.
“Hii ni
fursa ya kujikumbusha umuhimu wa amani duniani na kuacha kushabikia masuala ya
vita, bila kujua atahari zake,vita vinavyotea sasa hivi mashariki ya kati, Israel
na Marekani na Iran na maeneo mengine athari zinakuja kwetu mafuta yanapanda
bei,na mafuta ndio kila kitu na kusababisha kila bidhaa kupanda bei ni wakati
mzuri wa watanzania kuombea amani na usalama kwa mataifa mengine duniani”alisema
Kwa upande
wake Masood Daud Masood Imamu wa msikiti wa Dhi- Nureyn amewashukuru wale wote
waliojitolea kutoa sadaka hiyo ya ng’ombe wamepokea na kuomba wadau wengine
waweze kuwasapoti.
“Taaasisi ya
Dhi-nureyn ni taasisi inayosaidia watu wasiojiweza lakini pia yatima,hivyo
tunaomba wadau waweze kujitokeza kutusaidia kwa mahitaji mbalimbali na kusaidia
jamii na waislamu kwa ujumla”alisema
MWISHO.


.jpeg)
