RC KHERI AWATAKA WAISILAM KUSIMAMIA MAADILI NA KUJENGA MSHIKAMANO.
NA MATUKIO DAIMA MEDIA.
IRINGA.WAUMINI wa Dini ya Kiislamu Mkoani Iringa wameungana na Waislamu wengine duniani kusherehekea Sikukuu ya Eid Al-Adh'ha kwa kutekeleza ibada ya Sala ya Eid pamoja na kuchinja wanyama kwa mujibu wa mafundisho ya dini hiyo.
Baadhi ya waumini hao wamejitokeza kwa wingi kushiriki ibada sambamba na ufunguzi wa msikiti wa Masjid Faraj mjini Iringa.
Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James amesema kuwa sikukuu hiyo ni miongoni mwa sikukuu za kuchinja na kutoa zawadi kwa kushirikiana na jamii.
Alisema kuwa moja ya jukumu la msingi la tasisi ya kidini ni kusaidia kujenga mshikamano na kusimamia maadili“NI matarajio yangu msikiti huu mpya utaendelea kusimamia misingi umoja na mshikamano katika mji wa Iringa na kusaidia kusimamia maadili ya jamii ili tuwe na jamii bora yenye uadilifu,uaminifu na uwajibikaji usiokuwa na mashaka”alisema
Kheri James alisema kuwa Mwenyezi Mungu amewabariki waislamu kufikia Sikukuu ya Eid Al-Adh'ha hivyo waende kusherehekea kwa amani msikamano na upendo huku mkiwatendea watu wote matendo ya huuma na upendo katika jamii.
“Tunaoneshe namna tofauti ya kusherehekea sikukuu bila kufanya fujo, ghasia na mambo yanayomuuzi Mungu ili kila mmoja afurahi na sisi katika sherehe hii”alisema“Kwa niaba ya serikali ninawahakikishia usalama wa kutosha tukiwa na msaada wa Mwenyezi Mungu kama mlinzi wa kila jambo kuwa mji wetu utakuwa salama mwanzo wa sherehe hizi hadi mwisho”
Aidha amwapongeza wote walioshiriki na kusimamia ujenzi wa msikiti huo wamefanya kazi kubwa na nzuri kuhakikisha mji wa Iringa umepata msikiti mkubwa na wenye muonekano wa kipekee na nafasi ya kutosha.
“Msikiti huu umebadilisha mandhari ya mji wa Iringa, iringa ina maeneo mengi yanayotumika kama alama ya mji na sasa msikiti huu utatumika kama moja ya alama ya mkoa wa Iringa hii ni ishara kuwa kuna kitu kimpya kimeongezeka katika mji huu, hili ni jambo la shukrani kwa waliosimamia ujenzi huu”AlisemaKwa upende wake MCC Salim Abri Asas alisema Msikiti huo ni miongoni mwa misikiti mikubwa katika mji wa Iringa ambapo kila muumini anapaswa kushiriki katika ibada kwa ajili ya kumcha Mungu.
“Msikiti huu ulikuwa unasubiriwa na hamu na waamini wa mji wa Iringa leo umefunguliwa tunamshukuru Mwenyezi Mungu hivyo tuzidishe ibada kwa sababu msikiti ni waumini hivyo wajitokeze kufanya ibada kila siku”Naye Mwenyekiti wa Baraza kuu la Waislamu Tanzania,Mkoa wa Iringa Mussa wanguvu amewataka waumini kuutumia msikiti huo kufanya ibada na uko wazi kwa mmoja.
“Kinachotakiwa kufanyika ndani ya msikiti ni ibada na si vinginevyo watu wanaotaka kufanya siasa haturuhusu,kama kuna watu wanahitaji siasa waombe tuwajengee ukumbi ili waweze kufanya siasa zao”Wanguvu aliongeza kuwa msikiti huo unafanya misikiti kuongezeka mkoani hapo na kufikia 70 katika Manispaa ya Iringa,hivyo tunahitaji waumini wengi zaidi waweze kuitumia misikiti hiyo kwa ajili ya kufanya ibada.
MWISHO.
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
