VUNJABEI APIGA KAMBI ISIMANI KUOMBA KURA ZA EMANYELA MTATIFIKOLO
NA MATUKIO DAIMA MEDIA
Aliyekuwa mtia nia wa ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Fred Ngajiro maarufu kama Vunjabei, ameendelea kusaka kura za mgombea ubunge wa CCM Emmanuela Mtafikolo, katika uchaguzi mdogo wa marudio unaotarajiwa kufanyika Juni 1.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CCM Wilaya ya Iringa Vijijini, Vunjabei alisema kuwa akiwa mwana CCM anawajibu kuendelea kumnadi mgombea wa CCM Mtatifikolo ambae chama kimempitisha na kuwa mgombea huyo anauwezo mkubwa wa kuendeleza yote ya hayati Wiliam Lukuvi .
"Sisi kama watiania na wana CCM jukumu letu ni moja kusaka kura za CCM kila kona ya jimbo la Isimani ili ushindi wa kishindo kuonekana katika uchaguzi huo "
Alisema kuwa kwa dakika hizi za lala salama wana CCM wote wapo timu moja ya ushindi kusaka kura za kutosha na kuwa mgombea wao anamvuto mkubwa na uhakika wa ushindi ni mkubwa.
kwani alisema kuwa jukumu lake ni kuunga mkono uamuzi wa chama wa kumpitisha Emmanuela Mtafikolo kupeperusha bendera ya CCM kuwania kiti cha ubunge wa Jimbo la Isimani.
Hata hivyo aliwaomba wananchi wa jimbo la Isimani kwa ujumla wao kujitokeza kwa wingi jumatatu mapema zaidi kupiga kura kwa Mtatifikolo .
Kwa upande wao wana CCM akiwemo Augustino Mkomola wamepongeza uamuzi wa Vunjabei kuongeza nguvu ya kampeni katika jimbo hilo na kuwa uamuzi wake unaonesha kuvunjwa kwa makundi ndani ya CCM.
Uchaguzi huo mdogo unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Isimani na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, William Vangimembe Lukuvi.
Uchaguzi mgodo jimbo la Isimani unashirikisha vyama vingine vya siasa 16 ambavyo vimejitosa kuwania nafasi hiyo ya ubunge ili kuziba nafasi iliyoachwa wazi baada ya kifo cha William Lukuvi.


