TAWIRI WAENDESHA ZOEZI LA KUYAFUNGA MIKANDA YA VISUKUMA MAWIMBI MAKUNDI YA TEMBO KILOMBERO
Na. Matukio Daima Media ,Kilombero, Morogoro.
TAASISI ya Utafiti wa Wanyampori Tanzania (Tanzania Wildlife Research Institute- TAWIRI) imeanza zoezi la kuyafunga mikanda ya visukuma mawimbi makundi ya tembo Wilaya ya Kilombero, ikiwa ni matumizi ya Technolojia kusadia kufuatilia makundi ya tembo yanayoleta changamoto kwenye maeneo ya wananchi.
Zoezi hilo linaongozwa na Mtafiti na Daktari wa wanyamapori kutoka TAWIRI, Dkt. Mikidadi Mtalika huku pia wakishirikiana na TANAPA na Wadau wa Six-Rivers Africa.
"Teknolojia ya mikanda ya visukuma mawimbi inasaidia kuwa na uhifadhi endelevu wa tembo sambamba na usalama kwa jamii.
Aidha zoezi hili ni endelevu kwa mwezi huu kama ilivyo utafiti hauna ukomo" Imebainisha taarifa ya TAWIRI.
TAWIRI yenye makao yake makuu Njiro, Arusha, Ni taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, yenye jukumu la kufanya, kuratibu, na kusimamia tafiti za wanyamapori kwa uhifadhi endelevu na utalii nchini.
Lakini pia ikiwa na lengo kuu la kutoa ushauri wa kisayansi na taarifa sahihi kwa ajili ya usimamizi na uhifadhi wa viumbe hai.
Ikiwa imebobea katika shughuli za utafiti wa wanyamapori, mimea ya tiba asili, na ushauri wa kitaalamu, Inajulikana kama injini ya uhifadhi kupitia tafiti za Wanyamapori ambazo hutumika kwa ustawi wa Uhifadhi na kukuza Utalii nchini.

.jpg)