Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MBUNGE SHINGO AONGOZA ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU UKONGA

MBUNGE SHINGO AONGOZA ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU UKONGA

 

Na Matukio Daima Media

Mbunge wa Jimbo la Ukonga kupitia Chama Cha Act Wazalendo Bakari Shingo leo ameongoza zoezi la uchangiaji damu lililoenda sambamba na matembezi ya hisani kutoka Mombasa hadi viwanja vya Pugu kajiungeni lengo ni kuhamasisha jamii kujitokeza kuchangia damu.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo lililoandaliwa na ofisi ya Mbunge na Hospitali ya Rufaa ya Amana, Mbunge wa Jimbo hilo amesema kwamba bado kuna uhitaji mkubwa wa damu katika hospitali mbalimbali, hivyo wananchi wanapaswa kujitoa kuchangia damu ili iwepo akiba ya kutosha.


Amesema kuwa, ataendelea kushirikiana na Wananchi wa Jimbo hilo katika kuwaletea maendeleo pamoja na kushiriki kikamilifu katika masuala ya Afya.


"Tusidanganyike suala la kuchangia damu ni ibada, halina Vyama vya siasa, ukabila wala dini,damu tunayochangia itatusaidia sisi wenyewe, ndugu zetu na rafiki zetu wenye uhitaji wa damu" amesema Shingo.



Kwa upande wake, Afisa Tarafa Jimbo la Ukonga Kheri William, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amesema kuwa zoezi hilo limesaidia upatikanaji wa damu iatakayookoa maisha ya Watanzania.


Aidha amesema kuwa jitihada zinazofanywa na Mbunge huyo niza kipekee kwani ameamua kuwekeza kwa jamii kwa maono makubwa, ikiwemo kutoa mafunzo ya udereva wa magari, pikipiki na bajaji kwa vijana mbalimbali wa Jimbo hilo,hivyo lazima Afya zao zitunzwe.


"Mheshimiwa mbunge unafanya mambo ya kipekee sana,suala la uhitaji wa damu ni kubwa,dunia nzima wataalamu wamefanya utafiti lakini hakuna tafiti zilizoonesha kuwa tunaweza kutengeneza damu mbadala,


Amendelea kusema kuwa, anaweza mtu kukatika mguu akapata mguu wa bandia,lakini huwezi ukachanganya kitu chochote ili kupata damu,kwahiyo damu inapatikana kwa kuchangia ili kusaidia wagonjwa mbalimbali"amesema.

Nakuongeza "wenzetu wa benki ya damu kutoka Hospitali ya Rufaa ya Amana wametukumbusha kuwa bado kuna uhitaji mkubwa wa damu kutokana na ajali mbalimbali zinazotokea,pia wajawazito wanaojifungua kwa opresheni,hivyo zoezi hili la kuchangia damu ni muhimu sana kwa Wananchi".




Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3