BEI YA MAFUTA YAPAA KUFUATIA MVUTANO WA MAREKANI NA IRAN
May 10, 2026
Kauli kali za Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu Iran pamoja na majibu ya nchi hiyo zimeathiri kwa haraka masoko ya mafuta barani Asia Jumatatu asubuhi, na kusababisha kupanda kwa bei kwa takriban asilimia 3.
Mafuta ghafi ya Brent ya Bahari ya Kaskazini yalifikia dola 104.09 kwa pipa katika biashara za mapema Jumatatu asubuhi.