Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WAWILI WAFARIKI, 13 WAJERUHIWA AJALI YA BASI NA LORI MSEKE

WAWILI WAFARIKI, 13 WAJERUHIWA AJALI YA BASI NA LORI MSEKE

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA

IRINGA.Watu wawili wamefariki dunia na wengine 12 wamejeruhiwa katika ajali ya basi kampuni ya Classic lililokuwa likitokea Zambia Kwenda Jijini Dar es Salaam na lori iliyotokea katika eneo la Mseke kata ya Mseke mkoani Iringa.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa Alfredy Mwakalebela alisema kuwa ajali hiyo imetopkea majira ya saa 11 asubuhi.

Alisema kuwa wamepokea majeruhi 13 wa ajali ya basi na lori iliyotokea eneo la Mseke kati ya majruhi hao 10 wamepata majeraha ya kawaida na watatu wako katika hali mbaya.

“Majeruhi wote wamelazwa katika hospitali ya Rufaa na katika majeruhi waliozidiwa mmoja ni mwanamke mjamzito na mwingine ni mwanaume,vile vile tumepokea maiti mbili ambapo wote ni madereva mmoja dereva wa lori na mwingine dereva wa basi”alisema

Aliongeza kuwa kati ya majeruhi 12 wote ni raia wan chi za nje na mmoja ni mtanzania, majeruhi wanne raia wa Zambia na 8 raia wa Zimbabwe.

Akizungumza shuhuda wa tukio hilo Mussa Shaaban Musa alitoa kwa madereva wa malori kukagua break mara kwa mara kabla wanapoanza safari pia wapate muda wa kupumzika ili kuzuia uchovu unaoambatana na usingizi mwingi wawapo safarini.

Kwa upande wake Abdallah Abdi ambaye ni staff wa basi la Classic alisema kuwa dereva wa lori alilivaa basi hilo na katika kulikwepa lori hilo dereva wa basi akaamua kuingia porini.

“Basi lilikuwa na Abiria 30 waliokuwa wakitoka Zimbabwe kwenda Dar es salaam ambapo dereva wa basi hilo amevunjika miguu yote na mikono,dereva mwingine kavunjika miguu huku staff mmoja wa basi hilo amefariki hapo hapo wote raia wa Tanzania”alisema



Naye Mchungaji Dolnad Kiwanga wa kanisa la kirutheli KKKT dayosisi ya Iringa amesema ajali zimekuwa nyingi na kusababisha vifi vya watun na kuacha majeruhi wengi .

“Malori yameongezeka katika njia hii hivyo madereva wanapaswa kuwa waangalifu wanapokuwa barabarani kutokana na ongezeko la magari kutoka Dar kwenda Zambia hivyo umakini unatakiwa madereva wanapaswa kufuata sheria za barabarani na kuwa na ukaguzi wa brek wa mara kwa mara”

Hivi karibuni basi kampuni ya Shabibiy na lori la vinywaji lilipata ajali katika eneo la Tanangozi na kusababisha vifo vya watu watatno na mareruhi 28.

MWISHO.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3