Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WANANCHI ZAIDI YA ELFU KUMI BUKOBA WAONDOKANA NA ADHA YA MAJI

WANANCHI ZAIDI YA ELFU KUMI BUKOBA WAONDOKANA NA ADHA YA MAJI

 

Na Anold Deogratias Matukio Daima Media Kagera

Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoa wa Kagera umekamilisha uchimbaji na ujenzi wa visima 10 vya kuchotea maji katika kata nne za wilaya ya Bukoba, kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 500, hatua inayotarajiwa kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kufikia asilimia 74 na kunufaisha zaidi ya wananchi 10,000.

Akizungumza na waandishi wa habari meneja wa RUWASA wilaya ya Bukoba Mhandisi Evaristo Mgaya amesema kuwa visima vyote kumi zimekamilika na vimeanza kutoa maji ambapo kila kisima kitakuwa na uwezo wa kuhudumia wananchi zaidi ya 1,000.

“visima vyote vimekamilika vinatoa huduma kwa wananchi kila kisima kitahudumia wananchi elfu moja na kwa watu wa maeneo ya jirani na visima hivyo wananchi wanapata huduma bora za maji safi na salama”


Kwa upande wake meneja wa mradi wa Rukoma na Rubale Moshi Issac amewaomba wananchi kuendelea kutumia hudumu zao na kuwaunga mkono katika utoaji wa huduma ya maji kwa kuunganisha maji kwenye makazi yao.

“nitoe wito kwa wananchi waendelee kutumia huduma zetu  na waunganishe maji kwenye nyumba zao ili kuondokana na adha ya wananchi wengi kwenda sehemu moja kwa ajili ya kupata huduma ya maji lakini pia itawezesha kuokoa muda”

Nao baadhi ya wananchi wa akiwemo Diocres Willibard Mkazi wa Kyaitoke ameshukuru uwepo wa mradi huo katika maeneo yao na kueleza kuwa hapo awali walikuwa na shida kubwa ya maji na ilikuwa inawatesa hasa wanafunzi waliokuwa wanalazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo nyakati za kiangazi.

“nishukuru kutuleta mradi huu wa maji tulikuwa tunapata shida ya maji hasa kwa wanafunzi walikuwa wanatembea umbali mrefu kufuata maji na nyakati za kiangazi ilikuwa changamoto kubwa tulikuwa tunachota kwenye madimbwi”

Aidha mkazi huyo amewataka wananchi wenzake kulinda miundombinu ya maji ili iweze kutoa huduma ya maji kwa muda mrefu.

Naye Jesca Joseph mkazi wa kijiji Ombweya ameeleza kuwa walikuwa wanaangaika kupata huduma ya maji hivyo ameshukuru uwepo wa mradi wa maji katika Kijiji hicho.

“maji tulikuwa tunayafuata mbali na tulikuwa tunayachota kwenye madimbwi na tukinunua dumu moja ilikiuwa ni shilingi mia tano ila kwa sasa tunashukuru serikali kwa kutuletea huduma ya maji karibu”
Mradi huo wa uchimbaji visima umetekelezwa katika kata nne za Kyaitoke, Rukoma, Kibirizi na Ijuganyondo wilayani Bukoba mkoani Kagera, na umeanza kutoa huduma yam aji safi na salama.


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3