Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
AFYA YA AKILI TATIZO KWA VIJANA

AFYA YA AKILI TATIZO KWA VIJANA

 


NA EASTER KAMETA (UoI)

MATUKIO DAIMA MEDIA

Baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Ruccu waeleza sababu zinazopelekea uwepo wa matatizo ya afya ya akili na njia za kutatua tatizo hilo.


Matukio Daima imezungumza khatibu Maganga ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha Ruccu ameeleza  maana ya afya ya akili huku akitaja kuwa ni hali ya mtu kushindwa kujitambua anachokifanya pia ametaja baadhi ya sababu zinazo pelekea watu kupatamatatizo ya afya ya akili.


"Afya ya akili ni hali inayomfanya mtu  kushindwa kutambua anacho kifanya  kutokana kwamba anakuwa ameathilika kisaikolojia kutokana  na jambo  fulani ambalo likapelekea kushindwa kujiendesha mwenyewe na kuanza  kutumia  vilevi kupitiliza pia mtu kuwa na msongo wa mawazo kuoitiliza ."


 Kwa upande wake Grace Zekaria ambaye ni mwanafunzi wa Ruccu ameeza kuwa sababu zinazo weza kupelekea tatizo huku akitaja kuwa manyanyaso kutoka kwa wazazi  au watu wanao kuzunguka  na matumzi mabaya ya mitandao  kijamii  ni chanzo cha tatizo hili.


"Manyanyaso yakizidi kwa mtu yeyote yanaweza kupelekea kuathilika kisaikolojia na kujiona kama yeye si kitu katika jamii  pia matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii hupelea matatizo ya afya ya akili kutokana na kwamba baadhi ya vijana hutumia mitandao ya kijamii na kuangalia vitu visivyo na maadili   hivyo hufanya wao kupotea utimamu wa akili  Kutokana na kuwa wameathilika na matumizi  hayo ya mitandao"


Naye Ngombozi store ameeleza baadhi ya njia zinazo weza kusaidia katika kuepuka wimbi hili la matatizo ya nayotokana na afya akili huku akitaja kuwa serikali itoe elimu juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwa vijana  wa lika zote.


"Serikali itoe elimu  na mafunzo juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwa vijana kwani kwa sasa watu wengi wanao tumia simu kubwa ni vijana lakini baadhi yao  wanatumia vibaya mitandao hii kutokana na kwamba hawana elimu ya kutosha juu ya matumizi sahihi ya mitandao hivyo wanapaswa kupewa elimu ili kuepusha ongezeko la matatizo ya afya ya akili.


Pia Ester Amos ameeleza kuwa mtu aliye patwa na tatizo hili la afya ya akili anapaswa kukaa chini na kufanyiwa mahojiano na mwanasikolojia au daktari pia ametaja kuwa anapaswa kukaa na watu wengi ili kuweza kuepuka kuwa na msongo wa mawazo. 


" Mtu aliye athilika  na matatizo ya afya ya akili hapaswi kujitenga  ama kukaa mwenyewe anapaswa kukaa sehemu zenye watu wengi ili kuepusha msongo wa mawazo pia anapaswa kwenda kumuona daktari au mwanasaikolojia na kumueleza tatizo linalo mkumba ili aweze kumsaidia kwa kumpa ushauri na njia za kutatua jambo lake".

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3