BIASHARA YA PARACHICHI YANUFAISHA WENGI IRINGA
NA EASTER KAMETA (UoI)
MATUKIO DAIMA
Baadhi ya wafanyabiashara na wakulima wa parachichi mkoani Iringa waeleza namna wanavyo nufaika na bidhaa hiyo.
Akizungumza na Matukuo Daima Vivian Chalamila ambaye ni mkulima wa parachichi ameeleza kuwa kwa sasa uzalishaji umeongezeka huku akitaja kuwa ni kutokana na mahitaji makubwa ya watu kutoka soko la ndani na nje ya nchi.
"Uzalishaji wa parachichi umakuwa ukiongezeka kwasababu mahitaji yamekuwa mengi ya soko la ndani na nje pia watu wengi huitumia katika bidhaa hii katika matumizi tofauti tofauti kama vile katika utengenezaji wa bidhaa za viwandani na baadhi kutumia kama matunda ,kutokana na uhitaji huu na sisi wakulima tunajitahidi kuzalisha ili kuweza kukidhi mahitaji yetu na kukuza uchumi wetu na nchi kwa ujumla."
Aidha kwa upande wake Yusuph Msigwa ambaye ni mkulima ameeleza umuhimu wa wataalamu wanaotoa elimu juu ya biashara ya maparachichi na namna ya kufanya kilimo chake pia ameishukuru serikali kwa kutoa miche ambayo imekuwa ni njia ya kujifunzia namna ya kufanya kilimo hiki ili kuweza kupata mazao mengi.
"Wataalamu ni muhimu katika kutoa elimu juu ya biashara hii ya parachichi kwani inagharama nyingi na inahitaji uelewa wa kutosha ili kuweza kuimudu na tunaishukuru serikali yetu kwa kuwa na mchango chanya katika biashara na namna ya kufanya kilimo chake kwa kutoa miche na kutoa elimu juu ya kuitunza na baadae kuleta manufaa katika biashara ."
Vilevile Gabliel John ambaye no mfanya biashara ameeleza kuwa bidhaa ya parachichi imekuwa ni fursa kwa wa tanzania na kutaja kuwa baadhi ya watu wamejiajiri katika uuzaji wa parachichi ili kuweza kujipatia kipato chao.
"Kupitia zao hili la parachichi watu wengi wamepata fursa za ajira kwa kufanya biashara ya parachichi kulima na baadae kuuza na kisha kujipatia faida pia wengine wanafanya kazi za kusafirisha bidhaa hizi toka mashambani zinako limwa na kuleta mijini ambako ni sokoni kwaajili ya biashara ."
Piano Tumaini sapari amabye ni mfanyabiaahara wa bidhaa hii ameeleza kuwa bei wanazo kutana nazo katika kujumua kutoka kwa wakulima ni rafiki hivyo huwa fanya na wao kwenda kuuza kwa bei hizo ambazo ni za kawaida na haziwezi kumuumiza mfanya biashara wa kawaida na wateja .
"Bei mara nyingi hua inategemeana na mimi nimechukuaje mzigo toka shambani na usafirishaji ulikuwaje lakini kama nimechukua mzigo kwa bei inayo eleweka na nzuri na usafirishaji ukawa mzuri lazima niuze kwa bei ambayo itakuwa ni rafiki na si ya kumuumiza mteja na kupitia bei hizi husaidia kupelekea wote kupata faida sawa."

