Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
KILIMO CHA MBOGAMBOGA NI FURSA KWA BAADHI YA VIJANA

KILIMO CHA MBOGAMBOGA NI FURSA KWA BAADHI YA VIJANA

Na Ester Sebastian (UOI) Matukio Daima Media

Baadhi ya vijana wa mkoa wa Iringa waeleza faida ya kilimo cha mbogamboga ni moja ya fursa na wachangamkie  kwa wale vijana ambao hawana ajira itawasaidia kupata hela ndogo ndogo.

Mmoja wa mkulima wa bustani, Shabani Hamisi akieleza Matukio Daima kuwa Kupitia kilimo cha mbogamboga imemkwamua kiuchumi na kupelekea kupata genge lake la kufanyia biashara za mbogamboga.

"Vijana ambao hawana ajira  wasipende kukaa kiunyonge wafanye hata biashara ya bustani maana ni moja ya fursa maana mimi kupitia biashara ya mbogamboga inanisaidia kupata hela ndogo ndogo na mwisho wa siku kupata genge kubwa ya kufanyia biashara yangu" Alisema Hamisi

Naye msaidizi wake wa biashara yake, Lilian Shaa amesema alikuwa mdada wa nyumbani tu lakini Shabani alimshawishi na kumpa kazi katika kilimo chake na imempa fursa ya kupata ujuzi wa kulima mboga mboga pia na kupata hela ya kuanzisha biashara yake binafsi.

"Kupitia Shabani amenifanya nipate ujuzi wa kilimo cha mbogamboga na kunifanya kutokuwa tegemezi kwa wazazi wangu maana nilikuwa mdada wa nyumbani na kunipelekea kupata hela ya kuanzisha kibiashara changu" Alisema Shaa

Kwa upande wake Josephy Saimon, ambaye ni mnunuzi kupitia genge la Shabani amesema tangu amjue Shabani ni kijana anae penda kujaribu  biashara tofauti tofauti lakini kupitia kilimo cha mboga mboga yupo vizuri na watu wengi hupenda kununua mboga kwake.

"Tangu ni mjue Shabani ni kijana anae penda kujaribu na uthubutu kupitia kilimo cha mbogamboga yupo vizuri na kama akiona mboga inadawa hawezi kuwapa wateja wake hadi ile dawa ikiisha kwenye mboga yupo tofauti na watu wengine wanaofanya biashara ya mbogamboga" Alisema Saimon.

                                                    MWISHO

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3