UKARABATI MELI YA Mv.LIEMBA WASHIKA KASI
Meli ya Mv.Liemba ikiwa kwenye matengenezo
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
KAMPUNI ya meli Tanzania (TASHICO) imepokea injini mbili kwa ajili ya Meli ya Mv Liemba ambayo inafanyiwa ukarabati mkubwa huku Shirika hilo likieleza kuwa matengenezo hayo yanatarajia kukamilika mwezi Julai mwaka huu.
Meneja mradi wa ukarabati wa meli ya Mv.Liemba Mhandisi Elias John Kivara toka Kampuni ya meli (TASHICO)Akizungumza wakati Mkuu wa wilaya Kigoma,Dk.Rashid Chuachua akikabidhi mashine hizo kwa uongozi wa TASHICO ambapo Meneja mradi wa ukarabati wa meli hiyo, Mhandisi Elias John Kivara amesema kuwa kupokewa kwa mashine hizo eneo la mradi kunahakikisha kwamba ukarabati huo utakwenda vizuri na utakamilika katika kipindi kifupi kijacho.
Mhandisi Kivara alisema kuwa kwa sasa ukarabati huo umefikia asilimia 64 sehemu kubwa ya meli hiyo ikiwa imeshafanyiwa ukarabati na kwamba injini hizo zinatakapoanza kufungwa zitachukua wiki mbili kukamilika na kwamba mradi mzima wa ukarabati huo unatarajiwa kukamilika mwisho wa mwezi Julai mwaka huu.
Akikabidhi injini hizo kwa uongozi wa TASHIKO Mkuu wa wilaya Kigoma,Dk.Rashid Chuachua alisema kuwa wanaamini ukarabati huo ambao utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 32 utakamilika haraka kwani mashine hizo ndiyo zingeweza kukwamisha utekelezaji kwa wakati wa meli hiyo.
Dk.Chuachua ambaye alimwakilisha Mkuu wa mkoa Kigoma,Balozi Simon Sirro alisema kuwa kukamilika kwa meli hiyo kunakwenda kutekeleza mpango wa serikali wa kuufanya mkoa Kigoma kuwa mkoa wa kimkakati wa kiuchumi na biashara katika kutekeleza diplomasia ya uchumi.
Injini mpya ambazo zimepokelewa kwa ajili ya kufungwa kwenye meli ya Mv.LiembaAkizungumza katika hafla hiyo Meya wa manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya wananchi wa mkoa Kigoma alisema kuwa meli hiyo ni kichocheo kikubwa cha uchumi kwa wananchi wa mkoa huo na nchii za ukanda wa maziwa makuu kwani meli hiyo imekuwa kiunganishi kikubwa katika kuwaunganisha wafanyabiashara wa mkoa huo na nchii hizo.
Mkuu wa wilaya Kigoma



