Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
WANAWAKE IRINGA JITOKEZENI  HUDUMA YA SAMIA ARDHI KLINIKI -ZAINAB MWAMWINDI

WANAWAKE IRINGA JITOKEZENI HUDUMA YA SAMIA ARDHI KLINIKI -ZAINAB MWAMWINDI

 


NA MATUKIO DAIMA MEDIA

KUELEKEA maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika Machi 8 kila mwaka, wanawake mkoani Iringa, wamehimizwa kujitokeza kwa wingi katika huduma za 'Samia Ardhi Kliniki ili kunufaika na huduma mbalimbali za masuala ya ardhi. 

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi(UWT) Mkoa wa Iringa Zainab Mwamwindi alipotembelea banda la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Ofisi ya Mkoa wa Iringa 

Wanawake wa umoja huo walitembelea kliniki hiyo iliyoweka kambi katika viwanja vya Garden Manispaa ya Iringa inayotoa huduma mbalimbali za ardhi pamoja na elimu kwa wananchi. 

Kambi hiyo ilianza Machi 2, 2026 na inatarajiwa kufungwa Machi 7, 2026, ambapo Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaaenda na kauli mbiu " Haki na usawa kwa wanawake na wasichana,Msingi jumuishi kufikia Dira ya 2050.


Mwamwindi, alisema kuwa umiliki wa ardhi kwa mwanamke una mchango mkubwa katika kumwezesha mwanamke kujitegemea kiuchumi na kupata dhamana ya mikopo pamoja na kuwa kinga ya makazi au shughuli za kilimo pindi changamoto za kifamilia zinapotokea.

"bado kuna umuhimu wa kuendelea kuwahamasisha wanawake kujitokeza kumiliki ardhi kwani baadhi yao hukosa ujasiri au kunyimwa haki za mirathi kutokana na kukosa uelewa sahihi wa sheria na taratibu za ardhi hasa wenza wao wanapoondoka duniani au kutengana"

Alisema kuwa jutihada za serikali ni kumsaidia mwanamke na kumuinua ili asiachwe nyuma katika haki ya kumiliki ardhi pamoja na shughuli zingine za ujasiliamali.

Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Iringa Rehema Kilonzi alisema hadi sasa zaidi ya wanawake 130 wamefanikiwa kupata hati za ardhi kupitia kliniki hiyo huku lengo likiwa kuwafikia watu 300 kabla ya kukamilika kwa zoezi hilo.

Alieleza kuwa Kliniki ya Samia Ardhi ni mpango maalum unaolenga kuongeza idadi ya wanawake wanaomiliki ardhi ambapo kwa sasa takwimu zinaonesha kuwa ni takribani asilimia 28 pekee ya wanawake wanaomiliki ardhi.


" Mpaka sasa tumetoa hati za umiliki wa  ardhi 127 kwa wanawake kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Iringa ambapo ni sawa na asilimia 60 ya wanawake waliojitokeza kuchukua ardhi pamoja na kupata ushauri katika banda hili"

Alisema kuwa wanafurahia muamko mkubwa unaoonyeshwa na  wanawake katika uhitaji wa kumiliki ardhi pamoja na kupata ushauri kuhusu utatuzi wa migogoro ya ardhi.


Mpango huo ni sehemu ya jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuboresha upatikanaji wa huduma za ardhi kwa misingi ya haki, usawa na ujumuishi kwa makundi mbalimbali ya jamii, hususan yale yaliyo katika hatari ya kubaguliwa.

MWISHO.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3