Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
UWT MKOA WA  IRINGA YATOA MSAADA KITUO CHA WATOTO SAFINA STREET NETWORK  KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

UWT MKOA WA IRINGA YATOA MSAADA KITUO CHA WATOTO SAFINA STREET NETWORK KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

NA BERDINA MAJINGE ,MATUKIO DAIMA MEDIA.

Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2026, imetoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Safina Street Network kilichopo Mtwivila mjini Iringa, ikiwa ni sehemu ya kuonyesha upendo na mshikamano kwa watoto wenye uhitaji huku ikitoa wito kwa jamii kuendelea kujenga utamaduni wa kusaidiana na kuwajali watu wenye uhitaji.

Akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi msaada huo katika kituo hicho, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Iringa, Zainab Mwamwindi, amesema msaada huo pamoja  unalenga kuimarisha mshikamano, upendo na ustawi wa jamii kwa ujumla, huku akihimiza jamii kuendelea kuwa na moyo wa kusaidia na kuwajali watoto yatima pamoja na watu wengine wenye uhitaji katika jamii.

" Sisi kama wanawake tumeguswa kufika mahali hala kwa kuwa sisi ni wazazi na tumekuja kuwaona na kutoa msaada kidogo ili watoto wetu wazidi kustawi na kukua vyema"

Akisoma risala ya kituo cha safina mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo hicho Christian Mdongwe alisema kuwa wanakabilia na ukosefu wa makao ya watoto na vijana ambapo kituo hicho kinahudumu zaidi ya watoto 40 ambapo hawana makazi ya kuwaweka kwani nyumba wanayoishi wamepanga.

" Tunaomba serikali itutazame kutusaidia katika upatikanaji na maendeleo ya kiwanja chetu cha hekari 5 kilichopo mtaa wa Kigonzile kwa ajili ya ujenzi wa makao ya watoto pamoja na mahitaji yetu ya msingi" alisema

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3