Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MIGOGORO 60 YAPATIWA SULUHU SAMIA ARDHI KLINIKI KIGOMA

MIGOGORO 60 YAPATIWA SULUHU SAMIA ARDHI KLINIKI KIGOMA

 

Mkuu wa wilaya Kigoma Dk.Rashid Chuachua (katikati)  akiongoza kliniki ya Migogoro ya ardhi manispaa ya Kigoma Ujiji
Wananchi wa manispaa ya Kigoma Ujiji waliojitokeza kwenye kliniki ya kusikiliza migogoro ya ardhi kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
Watendaji wa idara ya ardhi ofisi ya Afisa Ardhi Mteule mkoa Kigoma na Manispaa ya Kigoma Ujiji wakishughulikia migogoro mbalimbali ya wananchi kwenye Samia Ardhi Kliniki mkoa Kigoma

Na Fadhili Abdallah,Matukio Daima Media Kigoma

MIGOGORO 60 ya aardhi imetatuliwa katika siku tatu za mpango wa kusikiliza kero za malalamiko ya ardhi maarufu kama Samia Ardhi Kliniki katika manispaa ya Kigoma Ujiji ikiwani sehemu ya maadhimisho kuekelea kilele cha siku ya wanawake duniani.

Mkuu wa wilaya Kigoma,Dk.Rashid Chuachua alisema hayo katika uwanja wa Kawawa Ujiji Mjini Kigoma ambako kliniki hiyo inaendelea na kueleza kuwa tangu Machi mbili mwaka huu kliniki hiyo ilipoanza jumla ya migogoro 90 ilikuwa imepokelewa imesikilizwa.

Dk.Chuachua alisema kuwa ipo migogoro ya ya mirathi  na mipaka iliyochukua muda mrefu ambayo ilimalizwa kwa watu wanaogombana kukubaliana baada ya mazungumzo yaliyosimamiwa na Mkuu huyo wa wilaya na hivyo wataalam kwenda eneo la tukio kubainisha mwisho wa mipaka ya kila mmoja,


Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa awamu hii ya kwanza ya kliniki hiyo itaisha tarehe saba mwaka huu kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake tarehe nane na kwamba kuanzia tarehe tisa kliniki hiyo itaendelea kwa ngazi ya wilaya hadi Machi 16 mwaka huu ikihusika kwenye kata na vijiji mbalimbali vya halmashauri ya wilaya Kigoma na Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Akizungumza wakati wa kliniki hiyo Afisa ardhi Mteule wa mkoa Kigoma, Elias Mwazembe alisema kuwa sehemu kubwa ya migogoro hiyo ni uelewa wa mambo ya wananchi kwani ipo migogoro ya ardhi ya masuala ya mirathi ambayo ipo mahakamani hivyo wao wanawaelekeza wahusika kuendelea na kesi zao mahakamani lakini wamekuwa wakitoa ushauri kwa mahakama uhalisia wa kupatia ufumbuzi wa migogoro hiyo.


Mwazembe alisema kuwa mingi ya migogoro ya mirathi kwenye ardhi inakuja kwenye suala la baadhi ya ndugu kutaka kuuza mali hizo huku baadhi ya ndugu wakitengwa kwwenye umiliki hivyo suala hilo huwa linarudishwa mahakamani ili sheria ya mirathi iweze kutekelezwa katika mgawanyo wa mali.


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3