Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
NAIBU WAZIRI WA MAKAZI NA UHIFADHI WA IRELAND KUFANYA ZIARA MKOANI ARUSHA

NAIBU WAZIRI WA MAKAZI NA UHIFADHI WA IRELAND KUFANYA ZIARA MKOANI ARUSHA

 

Na,Jusline Marco;Arusha

Naibu Waziri wa Makazi, serikali za Mitaa na urithi wa Kale wa Ireland Mhe. Christopher O'Sullivan anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi Mkoani Arusha kuanzia Machi 10, 2026,huku akitarajiwa kukutana na wadau wa masuala ya uhifadhi pamoja na Jumuiya ya Raia wa Ireland wanaoishi Mkoani Arusha.

Hayo yamesemwa leo Machi 09, 2026 na Balozi wa Jamhuri ya Ireland Nchini Tanzania Mhe. Nicola Brennan, wakati alipokutana na kuzungumza na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Makalla Jijini Arusha, ambapo amesema lengo la ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kiuchumi baina ya Tanzania na Jamhuri ya Ireland.

Wakati wa mazungumzo yao, Mhe. Makalla ameishuikuru Ireland kwa kuendelea kuwa mdau wa maendeleo nchini, akisema ujio wa Naibu Waziri huyo ni udhihirisho wa urafiki na ushirikiano wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili, ambapo ametoa rai kwa Ireland kuendelea kuwekeza na kutumia fursa mbalimbali za kiuchumi na kijamii zilizopo Mkoani Arusha.

Mhe. Makalla ameeleza pia kuhusu hali ya usalama na utulivu, akimtaarifu Balozi Brenan kuhusu ujenzi wa miundombinu ya barabara kwenye hifadhi ya Ngorongoro, akimueleza Balozi Brennan kuwa serikali kwasasa inajenga barabara ya tabaka gumu ili kuunganisha hifadhi mbili za Ngorongoro na Serengeti ili kuendelea kurahisisha shughuli za utalii kwa kuzifanya barabara hizo kupitika kwa muda wote.

Aidha Mhe. Balozi Brennan ameeleza mpango wa Ireland kuwekeza katika kuwezesha Kilimo cha mbogamboga na Bustani nchini Tanzania pamoja na fursa nyingine za kiuchumi na kijamii, akimshukuru Mhe. Makalla kwaniaba ya serikali kwa namna ambavyo serikali imeendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali na Raia wa Ireland waliopo nchini Tanzania, akiahidi kuendelea kupanua na kuendeleza ushirikiano zaidi na Tanzania katika kuwanufaisha wananchi wa pande zote mbili.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3