Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
CPA MAKALLA AHIMIZA USHIRIKIANO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO.

CPA MAKALLA AHIMIZA USHIRIKIANO KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO.

 

Na,Jusline Marco:Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha CPA Amos Makalla amehimiza umoja na ushirikiano wa dhati kati ya Wananchi, Wabunge, Wenyeviti wa Halmashauri, Meya wa Jiji na Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara za Viwango vya lami na Changarawe pamoja na kulinda na kutetea maslahi ya Mkoa wa Arusha.

Makalla ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara Mkoa wa Arusha, ametoa kauli hiyo leo Machi 09, 2026 wakati akifungua Mkutano wa 51 bodi hiyo, akiwashukuru wasaidizi wake katika ngazi mbalimbali kwa ushirikiano wao tangu kuteuliwa kwake, akisisitiza kuendelea kujitoa katika kuhakikisha malengo na dhamira njema ya Rais Samia suluhu Hassan kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha.

Aidha amesisitiza maelekezo yake ya Wakala wa barabara TANROAD kuendelea kuyatumia Mabaraza ya Madiwani zaidi katika kupokea changamoto za barabara kutoka kwa Madiwani kama njia sahihi ya kutambua mahitaji na vipaumbele katika Kata zao na kuweza kuzifanyia kazi.

"Ni kikao hiki pia kinachoweza kuazimia barabara za kupandisha hadhi na zipi za kujengwa kwa kiwango cha lami kama yalivyokuwa maelekezo ya Waziri Mkuu kwa barabara ya kuingia Hospitali ya Wilaya ya Arusha Dc, Moshono- ByPass, Karatu- Eyasi na Longido- Siha ili tutatue kero za barabara katika maeneo mbalimbali Mkoani hapa." Amesema Mhe. Makalla.

Pamoja na mambo mengine,kikao hicho  kimepokea taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya TARURA, TANROAD na NCAA kwa mwaka 2024/25 na 2025/26, mpango kazi kwa mwaka 2025/26, kupokea na kujadili bajeti ya matengenezo ya barabara, pamoja na maelekezo ya Waziri Mkuu ya kujengwa kwa barabara za kiwango cha lami na kupandishwa hadhi ya baadhi ya barabara katika Mkoa wa Arusha.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3