MDHARA YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA KATIKA ELIMU
NA EASTER KAMETA ( UoI)
MATUKIO DAIMA
Baadhi ya wanafunzi mkoani Iringa wameeleza madhara yanayo tokana na maendeleo ya Sayansi na Teknolojoa katika nyanja za kielimu .
Akizungumza na Matukio Daima Agripina Baraka ameeleza kuwa Teknolojia imepelekea udumavu wa akili ya mwanafunzi huku akitaja kua matumizi makubwa ya mitandao na vifaa vya kidigitali badala ya mijadala darasani kua ni chanzo cha udumavu huo.
" Mtumizi makubwa ya vifaa vya kidijitali badala ya majadiliano ya moja kwa moja darasani kwa mwanafunzi yameleta utegemezi mkubwa wa teknolojia ambapo unafanya wanafunzi wengi kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi wa akili zao na hivyo hupelekea udumavu wa akili ya mwanafunzi kutokana na matumizi makubwa ya vifaa kama kompyuta ,simu na mitandao.
Christian Titus ameeleza kuwa mitandao ya kijamii kama vile matumizi ya akili mnemba ni njia ambayo inapelekea mwanafunzi kuto kuwa na uwezo wa kufanya ubunifu wao binafsi na kukuza ujuzi pia ametaja kuwa teknolojia ni chanzo cha udanganyifu katika masomo.
"Kupungua kwa uwezo wa kufanya ubunifu kwa mwanafunzi ni kunatokana na Kutegemea sana majibu ya haraka kutoka akili mnemba kunaweza kupunguza ubunifu ,ujuzi na uchambuzi binafsi ,pia udanganyifu wa kitaaluma hii ni kutokana na kwamba Teknolojia inaweza kurahisisha udanganyifu kama vile kunakili kazi au kupata majibu mtandaoni ambapo unakua si ujuzi wa mwanafunzi"
Alizera Adamu ameeleza jinsi vifaa vya kidigitali vinavyo weza kupelekea usumbufu wakati wa masomo na wakati wa kujifunza pia ametaja kua vifaa hivi ni moja ya visababishi vya mmomonyoko wa maadili .
"Usumbufu wakati wa kujifunza Simu na kompyuta zinaweza kuwafanya wanafunzi kuhalibika kutokana na kutumia mitandao ya kijamii vibaya pia kuiga vitu visivyo faa,mavazi yasiyo na maadili pia matumizi ya dawa za kulevya ambapo huweza kupelekea mmomonyoko wa maadili"
Wakati Alon Mwachembe ameeleza baadhi ya athali za kiafya ambazo mtumiaji wa mitandao ya kijamii atazipata iwapo atatumia kupitiliza huku akitaja baadhi ya magonjwa mama vile macho, kichwa na mgongo
"Mitandao ya kijamii hususani kompyuta husababisha matatizo ya kiafya ambayo yanaweza kuwapata watumiaji wa vifaa hivi kutokana na matumizi ya muda mrefu kama vile matatizo ya macho au maumivu ya mgongo kichwa kuuma mara kwa mara ambapo huweza kupelekea mwanafunzi kuto kuona vizuri awapo darasani"

