WAKULIMA KAGERA WAPEWA SOMO KILIMO MSETO KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI
Na Anold Deogratias Matukio Daima Media Kagera
Wakulima mkoani Kagera wamesahuria kulima kilimo mseto ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuepukana na hasara zinazoweza kujitokeza endapo mkulima atakuwa amelima zao la aina moja na yakatokea mabadiliko ya hali ya hewa kama ukame.
Ushauri umetoliwa na mkurugenzi wa shirika lisilokuwa la kiserikali linalojiusisha na kilimo na mazaingira la Smart Farmer Bw.Clement Mtui wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa kilimo mseto kinachohusisha mazao mengi ndani ya shamba moja kinasaidia kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi endapo zao moja likiharibika mengine yanaweza kuhimili mabadiliko hayo.
kilimo mseto kinasaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kilimo hiki kitamsaidia mkulima kuepukana na hasara endapo yatatokea mabadiliko hayo kama ukame au mvua kuwa nyingi mazoa mengine yanaweza kustahili hali hiyo”
Aidha katika hatua nyingine Bw.Mtui amesema kuwa shirika hilo linampango wa upandaji wa milioni moja ambayo itagawiwa kwa wakulima 100, ya matunda nay a kivuli ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi wilayani Karagwe mkoani Kagera.
“pia tunampango wa upandaji wa miti ya matunda na kivuli ambayo tutaigawa kwa wakulima na kuipanda hali itakayosaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi lakini pia kuimalisha afya za wananchi wilayani Karagwe”
Nao baadhi ya wakulima wilayani Karagwe akiwemo bw. Sadick Mohamed amesema kulima mazao mchanganyiko katika shamba moja kumemsaidia kuongeza kipato pamoja na kuwa na uhakika wa chakula.
“kilimo ni ajira tosha mimi naendesha maisha yangu kupitia kilimo nimejenga ninasomesha watoto kupitia kilimo na kilimo mseto ni kizuri, ukikosa kwenye mahindi unapata kwenye maharage au migomba”
Naye Bw.Longino George amesema kuwa kulima zao moja katika shamba moja kuna hatari ya mkulima kupata hasara endapo zao hilo litaharibika kutokana na mabadili ya hali ya hewa kama ukame.
ukilima zao katika shamba moja na usichanganye kitu kingine basi likiharibika limeharibika una hatari ya kukosa yote, lakini kama umelima kwa kuchanganya mazao mengine yanayovumilia ukame unanufaika unaweza kupoteza huku ukanufaika na kwingine”
Hata hivyo katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa shirika la Smart Farmer limezindua mradi wa kuwaelimisha wakulima juu ya kilimo mseto, na wanalengwa kuwafikia wakulima wapatao 8000 kwa muda wa miaka 3.



