KUELEKEA UZINDUZI WA WAZOHURU APARTMENTS VIFAA VYA MICHEZO VYA MIL 4 VYATOLEWA KWENYE SHULE ZA MSINGI
Na Lilian Kasenene.
Matukio DaimaApp
KAMPUNI ya Wazohuru Media Group Limited amechangia vifaa vya michezo vya thamani ya shilingi milioni 4.2 kwenye shule za msingi katika Manispaa ya Singidaikiwa ni kuelekea uzinduzi wa WazoHuru Air BnB Apartments.
Vifaa hivyo vya michezo ni pamoja na jezi Jozi moja yenye jezi 16 na mpira mmoja katika shule ya Msingi Tumaini Viziwi, shule ya msingi Ukombozi, shule ya Kindai, shule ya msingi Sumaye, shule ya msingi Mtipa na shule ya msingi Unyankae.
Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo, Afisa Mtendaji Mkuu wa WazoHuru Media Group Ltd Mathias Canal alisema kuwa Lengo kuu la zoezi ni kuhamasisha michezo mashuleni, kukuza vipaji vya wanafunzi, pamoja na kuchangia maendeleo ya afya na ustawi wa watoto.
Canal alieleza kuwa pamoja na mambo mengine lakini pia kampuni yake imekabidhi vifaa hivyo vya michezo ikiwa ni sehemu ya mrejesho katika jamii baada ya kukamilika kwa ujenzi wa majengo 7 ya WazoHuru Apartments yaliyopo Mtaa wa Unyankae - Miembeni Manispaa na Mkoa wa Singida.
Mathias alibainisha kuwa March 28 Machi 2026, mradi huo wa eneo la makazi ya kisasa utazinduliwa ambapo mgeni rasmi katika tukio hilo atakuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego.




