Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
KITIKI KULETA MAPINDUZI YA KILIMO KWA WAKULIMA WADOGO

KITIKI KULETA MAPINDUZI YA KILIMO KWA WAKULIMA WADOGO

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma


SHIRIKA la Chakula la Umoja Mataifa (WFP) limekabidhi zana za kilimo zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 50 kwa vikundi vitano vya wakulima katika wilaya za Kasulu, Kibondo na Kakonko ili kubadilisha kilimo cha wanachama wa vikundi kufanya kilimo cha biashara na kuondokana na kilimo cha kujikimu.


Vikundi hivyo vimekabidhiwa zana hizo baada ya kushinda wazo la uandishi bora wa miradi ya kilimo biashara kwa mwaka 2025/2026 kupitia mradi wa kilimo tija Kigoma (KITIKI) unaotekelezwa na WFP kupitia ufadhili wa Shirika la maendeleo la serikali ya Korea Kusini (KOICA) ambapo mwaka wa fedha 2024/2025 kiasi cha shilingi milioni 93 kilitolewa.


Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Meneja wa KITIKI (WFP), HYOYEOL LEE alisema kuwa sambamba na kukabidhi zana hizo kwa vikundi hivyo vitano pia  wakulima binafsi saba wamefanikiwa kupata zana za kilimo ikiwemo vifaa na mashine za umwagiliaji,mashine za kupandia, kuwekea mbolea na kupukuchulia mahindi.


Kwa upande wake Mwakilishi wa Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Shirika la World Vision, Eric  Kidohela alisema kuwa kutekelezwa kwa mradi huo na kutolewa kwa vifaa hivyo kutaleta mabadiliko makubwa ya kilimo kwa wanufaika hao kufanya kilimo chao kuwa cha biashara na kuwa chenye tija kubwa.


Naye Isack Msumba,  Afisa mradi kutoka Shirika la Good Neighbors Tanzania alisema kuwa katika mradi huo wanahusika kwa kiasi kikubwa na utafutaji wa masoko na kwamba mradi huo utakuwa chachu kwa wakulima mkoani Kigoma kubadilisha kilimo chao kuwa cha biashara na chenye tija ambacho kitachochea watu wengi kuingia kwenye kilimo.

Akieleza mipango ya serikali kuhusu kilimo chenye tija mkoani Kigoma Afisa Kilimo kutoka Sekretariet ya mkoa Kigoma,James Peter alisema kuwa upo mpango wa kilimo wa mwaka 2020/2050 na mpango wa kilimo wa 2030/2050 ambayo yote inalenga kuimarisha kilimo na kuwainua wakulima wadogo kuongeza uzalishaji na kukifanya kilimo chao kuwa cha kibiashara.



Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3