BILIONI 1.2 KUTUMIKA KUZUIA UCHAFUZI ZIWA TANGANYIKA
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
WAJASILIAMALI wadogo mkoani Kigoma wanaofanya shughuli za ukusanyaji taka za plastiki na chuma chakavu zinazorejeshwa ili kutengeneza bidhaa wanatarajia kunufaika na ruzuku ya shilingi Bilioni 1.2 zinazotolewa na Shirika la Cathoric Relief Services (CRS) ikiwa ni mradi wa kuzuia uchafuzi katika ziwa Tanganyika (VOICES).
Mratibu wa Shirika la CRS ofisi ndogo ya Kigoma, Sinyonzile Samwel akizungumza katika mkutano na wajasiliamali hao uliofanyika mjini Kigoma alisema kuwa Shirika hilo kupitia mradi VOICES limefungua dirisha la maombi kwa awamu ya pili kwa vikundi mbalimbali vinavyojishughulisha na biashara ya ununuzi na ukusanyaji wa taka za plastiki na chuma chakavu.
Samweli alisema kuwa katika madirisha haya mawili likianza la awali mwaka jana na hili lililofunguliwa Machi 25 jumla ya shilingi Bilioni 1.2 zimetengwa kwa wajasiliamali ambao maandiko yao yatakidhi vigezo kupata mkopo huo kwa wakati huu ambapo kiwango cha kiasi gani kikundi kinatapa kinatokana na andiko mradi la kikundi husika.
Mratibu huyo alisema kuwa mradi huo ulioanza mwaka 2023 umekuja kunusuru ongezeko kubwa la taka hasa za plastiki ambazo kwa kiasi kikubwa haziozi zinazoingia kwenye ziwa Tanganyika na kuleta athari kwa mazingira na kusababisha mabadiliko ya tabia nchii hivyo mrai huo kwa sehemu yake unajaribu kukabiliana na changamoto hiyo.



