Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
DC KISSA:WANAWAKE ACHENI UOGA KUFANYA BIASHARA YA MAZAO YA MISITU ‎

DC KISSA:WANAWAKE ACHENI UOGA KUFANYA BIASHARA YA MAZAO YA MISITU ‎

 

Mkuu wa wilaya ya Makete Kissa Kasongwa kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe amewataka wanawake kuondokana na dhana ya kuwa uwekezaji katika sekta ya Misitu haulipi kwa kuwa miti inachukua muda mrefu mpaka kuvuna.

‎Katika Jukwaa la wanawake katika sekta ya Misitu Mwaka 2026 lililofanyika Mjini Makambako mkoani Njombe kwa ufadhili wa mradi wa Forland kupitia Serikali ya Finland na Tanzania,Kissa amesema changamoto ya kuchelewa kuvuna miti isiwakatishe tamaa wanawake kwani miti ni Pesa.


‎Awali Mratibu wa mradi wa Forland kitaifa Bi. Emma Nzunda Toka wizara ya maliasili na  utalii anasema hivi sasa wanawake wameanza kuingia kwenye shughuli za Misitu ikiwemo upandaji, uvunaji Hadi biashara ya mbao licha ya changamoto mbalimbali kuwakabili. 

‎Kwa niaba ya mkurugenzi wa Misitu na Nyuki  Dokta Siima Bakengesa Amesema Takribani hekta 48 Elfu za Misitu nchini sawa na asilimia 50 zimekuwa zikitumika kuliingiza mapato Taifa na mtu Mmoja Mmoja wakiwemo wanawake ambao wameingia kwenye sekta hiyo hivi sasa.


Kwa upande wao baadhi ya wanawake wanaojishughulisha na biashara ya mazao ya Misitu akiwemo Joyce Mpogole,Upendo Lutumbi na Atukuzwe Mtuta wamesema sekta hiyo Ina fursa nyingi ambazo inapaswa kuchangamkiwa licha ya kuwapo kwa baadhi ya changamoto kadhaa zikiwemo za kikodi.


Wanawake Toka mikoa ya Njombe,Iringa,Ruvuma na Lindi wameshiriki katika Jukwaa Hilo lililokwenda sambamba na Kauli mbiu ya  "Kufunguka fursa kwa wanawake kuongoza na kufanikiwa katika mnyororo wa thamani wa Misitu.



Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3