WAZALISHAJI WA MICHE YA KAHAWA KAGERA WATAKIWA KUONGEZA KIWANGO CHA UZALISHAJI
Na Anold Deogratias
Matukio Daima Media Kagera
Wazalishaji wa miche ya kahawa mkoani Kgera wametakiwa kuongeza kiwango cha uzalishaji wa miche hiyo ili kukidhi mahitaji yanayotakiwa kwa sasa ya miche milioni 30, hali itakayosaidia kukuza uchumi wa wananchi na mkoa wa Kagera kupitia zao la kahawa.
Wakizungumza katika kikao cha ushauri na maendeleo mkoa wa Kagera (RCC) wajumbe wa kikao hicho wamesema kunahitajika uzalishaji zaidi wa miche ili kuendana na uhitaji uliopo kwa sasa na pia wametaka ufanyike ufuatiliaji kuhakikisha wazalishaji wa miche hiyo wanatimiza lengo halisi la miche waliomba kuzalisha.
Mbunge wa jimbo la Muleba Kusini Mhe.Oscar Kikoyo amesema kuwa licha ya takwimu kuonyesha kuwa uzalishaji wa miche hiyo kwa sasa ni milioni kumi ila bado kuna uhaba mkubwa wa miche ya kahawa katika wilaya ya Muleba.
tumesikia hapa wasilisho kwamba uzalishaji kwa sasa ni miche milioni kumi ila mimi kwangu kwa wananchi ni ugomvi, wananchi wanahitaji miche haipatikani sasa naomba mkoa na kikao hiki tuongeze uagizaji wa miche kupitia halmashauri zetu
Kwa upande wake mbunge wa Biharamulo Magharibi Mhandisi Ezra Chiwelesa ametaka ufuatiliaji zaidi kwa watu waliokabidhiwa jukumu la kuzalisha miche hiyo ili kuhakikisha wanatimiza lengo la miche walioomba kuzalisha na kuepuka kuiingizia serikali hasara.
“tunahitaji ufutiliaji zaidi kwa wazalishaji wa miche ya kahawa mtu anaomba kuzalisha miche milioni moja hakuna mtu wa kuhakikisha kuwa kiwango alichoomba kuzalisha anakifikia mtu anaomba kuzalisha miche milioni kumi unakuta anazalisha laki tano
Kwa upande wake Katibu tawala msaidizi Uchumi na uzalishaji mkoa wa Kagera Isaya Tendega amesema kuwa uzalishaji wa miche kwa sasa ni milioni kumi ila mahitaji ni miche milioni thelathini na kwamba wataakaa na bodi ya kahawa na wazalishaji kuhakikisha wanazalisha kulingana na mahitaji.
mhe mwenyekiti naomba tulichukue hili ni kweli tunakubaliana kiwango cha miche kinachozalishwa na kusambazwa kwa wananchi ni kidogo kuliko mahitaji kwa mfano msimu huu mpaka January uzalishaji wa miche ni milioni kumi na mahitaji ni miche milioni thelathini
Katika hatua nyingine Bw.Tendega emeelezwa kuwa wataalamu wanendelea kufanya utafiti ili kuona jinsi ya kukabiliana na mdudu aitwaye Bungua Mweusi ambaye amekuwa akishambulia mibuni hivyo kuhatarisha uzalishaji wa zao hilo mkoani Kagera.
Mpaka kufikia Mwezi January 2026 mkoa wa Kagera umezalisha tani 54,202 za kahawa kwa thamani ya shilingi billion 256.4, huku halmashauri zikikusanya ushuru wa shilingi bilioni 7.69.



