MBUNGE MWANYIKA AGAWA MICHE 200 YA PARACHICHI UMAGO S/M UWEMBA
Ili kukabiliana na changamoto za Udumavu na uchumi kwa watoto mkoani Njombe Mbunge wa Jimbo la Njombe mjini Deodatus Mwanyika amegawa Miche 200 ya Parachichi kwenye shule ya msingi Umago kata ya Uwemba Halmashauri ya mji wa Njombe mkoani Njombe na kuipanda.
Akizungumza mara baada ya Kushiriki zoezi la upandaji miti hiyo Mbunge Mwanyika amesema anatamani kuona miti hiyo inakwenda kuwakomboa watoto na Udumavu kwa kupata Lishe Bora pamoja na kujiongezea kipato kupitia mradi wa Parachichi.
Awali Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Umago Happy Kawogo ameahidi kusimamia miti hiyo Hadi itakapoleta matokeo chanya
Naye Ofisa elimu Sekondari Halmashauri ya mji wa Njombe Rehema Nswila amesema mkakati wa kukabiliana na changamoto za Lishe unapaswa kuendelea kuungwa mkono na wadau wote kama anavyofanya Mbunge Mwanyika.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Uwemba na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Umago wanakiri kutunza miti hiyo kwani ni mradi mzuri kwa watoto.
.jpeg)

