RC KIDO ASISITIZA UBUNIFU KATIKA UKUSANYAJI WA MAPATO KAGERA
Na Anold Deogratias Matukioa Daima Media Kagera
Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali Yahya Ramadhan Kido amezitaka halmashuri kuongeza umakini katika ukusanyaji wa mapato ili kuwezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mkoa huo.
Akizungumza katika kikao cha ushauri na maendeleo cha mkoa (RCC) Kanali Kido amezitaka halmashauuri kupitia shughuli za kilimo, Uvuvi, Mifugo na biashara kuongeza ubunifu katika kukusanya mapato ya ndani kutokana na ushuru unaotokana na sekta hizo.
“kwa kuwa mkoa wetu una fulsa kupitia kilimo, uvuvi, biashara na mifugo kupitia halamashauri zetu tuongeze ubunifu katika kusimamia sekta hizo ili zitoe matokeo chanya na pia nisisitize ubunifu katika ukusanyaji wa mapato ili kutekeleza miradi ya maendeleo”
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa ametaka usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo ili iendane na fedha halisi iliyotumika na ihudumie wananchi kwa wakati na pia amewasisitiza watumishi kufanya kazi kwa uweledi, uaminifu na kwa kufuata sheria na taratibu zilizopo.
“nisisitize usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo katika mkoa wetu ili fedha iliyotumika ionekane katika miradi inayotekelezwa na kuwaondqelea adha wananchi”
Awali akiwasilisha rasmu ya bajeti ya mkoa wa Kagera kwa mwaka wa fedha 2026/2027 katibu tawala msaidizi upande wa uchumi na mipango Cosmas Alex,
amesema mkoa wa Kagera unatarajia kutumia kiasi cha shilingi bilioni 797.07 kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo na matumizi ya kawaida.
“mhe mwenyekiti mkoa unaomba kuidhinishiwa shilingi bilioni 797.07, kati ya hizo fedha za maendeleo, fedha za mishahara na matumizi mengineyo ni shilingi billion 523, na fedha hizi ni kutoka serikali kuu ambapo ni shilingi bilioni 464.
Hata hivyo katibu tawala huyo ameongeza kuwa mkoa unatarajia kukusanya mapato ya shilingi bilioni 58.4 kutoka katika halmashuri za mkoa wa Kagera.


