Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
POLISI YAWASAKA WANAWAKE WALIOMSHAMBULIA MWENZAO KWA MWIKO

POLISI YAWASAKA WANAWAKE WALIOMSHAMBULIA MWENZAO KWA MWIKO



Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Dodoma

JESHI la Polisi nchini Tanzania limesema limeanza kufanya uchunguzi kuhusiana na picha mjengeo inayosambazwa kupitia mitandao ya kijamii wakionekana wanawake wawili wakimpiga mwanamke mmoja kwa kutumia mwiko na kumshambulia kwa maneno kwa madai ya kudhalilishwa na mhanga wa tukio hilo kupitia mtandao Facebook.

Taarifa ya Polisi iliyotolewa leo Jumatatu Februari 09, 2026 na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, (DCP) David Misime imeeleza kuwa katika Picha hiyo mjongeo, wanawake hao wamesikika wakihoji sababu za mmoja wao kudhalilishwa kwenye Mitandao ya kijamii kuwa amekuwa akiiba mabwana (Waume) za watu

Jeshi la Polisi kupitia taarifa yake hiyo limetoa wito kwa yeyote anayewafahamu wanawake hao kuwasilisha taarifa zao kwa njia anayoona inafaa na rahisi kwake ili kuweza kuwafikia na kuwakamata ili kuwachukulia hatua za kisheria.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3