Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
MCH. TINGA ATINGA OFISINI RASMI WILAYA UYOLE.

MCH. TINGA ATINGA OFISINI RASMI WILAYA UYOLE.

 


TAZAMA VIDEO BOFYA HAPA

Na Josea Sinkala, Mbeya.

Mwenyekiti wa Kanisa la Moravian Tanzania wilaya ya Uyole Godfrey Tinga, amepokelewa rasmi katika wilaya hiyo na kuahidi kuendeleza kazi ya MUNGU na kuimarisha uchumi wa Kanisa na waumini kwa ujumla.

Mch.Tinga amepokelewa rasmi na waumini wilaya Uyole kuwa Mwenyekiti wa Kanisa la Moravian wilaya hiyo, ibada iliyofanyika katika Ushirika wa Ibala Uyole kati.


Akizungumza baada ya ibada hiyo, Mwenyekiti huyu mpya wa wilaya ya Uyole Kanisa la Moravian Jimbo la kusini magharibi Mchungaji Godfrey Tinga akiwa ameambatana na mkewe na viongozi mbalimbali, ameahidi kuendeleza huduma ya ki-Mungu na kusaidia kuinua uchumi wa Kanisa na waumini wilayani Uyole.

Pia amewaomba waumini wilayani humo kumpa ushirikiano pamoja na viongozi wenzake ili kuendeleza kazi ya MUNGU.

Viongozi mbalimbali wamehudhuria ibada hiyo akiwemo Mwenyekiti wa kanisa hilo wilaya ya Mbeya mchungaji Greenwell Sinkwembe ambapo viongozi mbalimbali wakimemo wenyeviti wa wilaya katika kanisa la Moravian Jimbo la kusini magharibi walichaguliwa kisha kupangiwa vituo vya kazi.


 Ibala uliopo jijini Mbeya imeongozwa na mwenyekiti wa dinari ya Uyole Mchungaji Luka Mtafya.

Ibada hiyo imehudhuriwa na Mwenyekiti wa Wilaya ya Mbeya, Mchungaji Greenwell Sinkwembe ambaye katika mahubiri yake amesisitiza umuhimu wa uongozi unaojengwa juu ya misingi ya upendo, unyenyekevu na mshikamano wa waumini, amewahimiza viongozi na waumini kushirikiana kwa karibu katika kuimarisha huduma za kanisa na kukuza maisha ya kiroho ndani na nje ya kanisa.


Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3