Kwa Habari za kitaifa, Kimataifa, Michezo, Burudani,Uchambuzi na matangazo. Matukio Daima Blog, Ni yetu Sote!
KUNA MAFUA MAKALI NA COVID 19 TANZANIA.

KUNA MAFUA MAKALI NA COVID 19 TANZANIA.

 

Wizara ya Afya Nchini Tanzania imetoa tahadhari juu ya uwepo wa mafua makali ya Influeza pamoja na UVIKO-19 (COVID 19) na kuwataka Wananchi kuchukua tahadhari kubwa.

Taarifa ya Wizara hiyo imesema kutokana na takwimu za ufuatiliaji zilizofanyika kwa kipindi cha mwezi Novemba hadi Aprili ongezeko kubwa la mafua makali ya INFLUEZA na UVIKO-19 hutokea hapa Nchini na Duniani.

Wizara imewataka Watanzania kuchukua tahadhari zifuatazo

kufunika pua na mdomo wakati wa kukohoa au kupiga chafya.

kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono ili kuepuka misongamano isiyo ya lazima.

Kuvaa barakoa unapokuwa na dalili, unapokuwa karibu na mtu mwenye dalili au ukiwa kwenye maeneo yenye msongamano.

Kuzingatia usafi binafsi na wa mazingira

Kuwahi katika kituo cha kutolea huduma za afya kupata matibabu stahiki.

kuepuka kujitibu au kutumia Antibiotiki bila ushauri wa Watalaam wa afya.

Aidha Wizara ya Afya imeeleza magonjwa hayo huambukizwa na kuenezwa kupitia majimaji kutoka kwenye mfumo wa njia ya hewa wa Mgonjwa mwenye maambukizi na husambaa wakati wa kukohoa, kupiga chafya au kuzungumza.

Imeongeza kuwa mafua makali ya Influenza na UVIKO-19 huweza kuenezwa kwa kugusa mazingira yaliyochafuliwa na majimaji yanayotoka kwa mgonjwa ambapo dalili za magonjwa haya ni homa kali, kikohozi, maumivu ya kichwa na mwili, mafua,

kuwashwa koo na uchovu.

Sponsored ads

Mid 1

Mid2

Ad3